habari


Yanga SC waifumua Kagera Sugar 3-0 na kuchumpa Nafasi ya pili ya Msimamo wa Ligi kuu.

1
Golikipa wa Kagera Sugar Ramadhani Chalamanda akipatiwa huduma ya kwanza Uwanjani.
 
Yanga SC imerudi nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara 2017/2018  baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar jioni ya leo March 9, 2018 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Ushindi huo sasa unaifanya Yanga SC kufikisha pointi 43 baada ya kucheza mechi 20, sasa ikizidiwa pointi tatu tu na vinara, Simba SC.
 
Katika mchezo huo ,mabao ya Yanga SC yalifungwa na Ibrahim Ajib dakika ya 53 kufunga kwa penalti baada ya beki Mzanzibari wa Kagera Sugar, Adeymum Saleh Ahmed kuunawa mpira kwenye eneo boksi.

MECHI%2B1
Ibrahim Ajib akinyoosha mikono juu kushangilia baada ya kuifungia Yanga SC bao la kwanza.
 
Goli lingine likafungwa na Yussuph Mhilu dakika ya 75 na Juma Shemvuni aliyemfunga kipa wake, Ramadhani Chalamanda katika harakati za kuokoa mpira uliopigwa na kiungo wa Yanga SC, Yusuph Mhilu aliyetokea benchi cha pili.
MECHI%2B2
Mabingwa hao wa Tanzania,Yanga SC watarudi uwanjani Jumatatu March 12, 2018 kumenyana na Stand United Uwanja wa Taifa, kabla ya kusafiri kwenda Botswana kwa mchezo wa marudiano na Township Rollers Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika, ambako wanatakiwa kushinda 2-0 waingie hatua ya makundi, baada ya kufungwa 2-1 Jumanne Dar es Salaam.

Post a Comment