habari

Uganda yazifungia Redio zaidi ya 20 kwa kutangaza 'Uchawi'.

 Nchini Uganda kuna mtandao mpana wa vituo vya redio vinavyofikia 270, hali ambayo inavilazimu baadhi yao kupokea matangazo kutoka kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi kama waganga.

Tume ya mawasiliano nchini Uganda, UCC, imefungia zaidi ya vituo 20 vya redio vya masafa ya FM kwa tuhuma za kutangaza 'uganga wa kienyeji, uchawi na kuwatapeli wananchi.'

Hatua hiyo inafuatia onyo la awali walilopewa la kuwatahadharisha kurusha matangazo ya waganga wa kienyeji.

Tangazo hilo la kufungiwa vituo vya redio 23 limetolewa March 27,2018 jioni na mwenyekiti wa Tume ya Mawasiliano Godfrey Mutabazi.

Bwana Mutabazi ameshutumu redio hizo kutumiwa na waganga wa kienyeji kuwatapeli wananchi na kuvunja sheria.

Redio hizo zimekuwa zikiwapa vipindi waganga hao wa kienyeji kutangaza uganga wao, huku wakiwaambia wananchi kutuma fedha kupitia njia ya simu za mikononi.

Nchini Uganda kuna mtandao mpana wa vituo vya redio vinavyofikia 270, hali ambayo inavilazimu baadhi yao kupokea matangazo kutoka kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi kama waganga.

(BBC)

Post a Comment