habari


Rulenge Bingwa wa Kombe la Polisi Jamii 2018.

29527150_1808040835902485_1468724124_o
 Mkuu wa Polisi wilayani Ngara Abeid Maige akielezea mafanikio ya Kombe la Polisi Jamii 2018 kuwa yamekuza mahusiano kati ya Polisi na Jamii kupitia kauli mbiu ya KATAA UHALIFU,FICHUA WAHALIFU  na jumla ya 18 zilishiriki mashindano hayo.
29634525_1808040995902469_25108630_o
Kikosi cha Mabingwa wa Polisi Jamii Cup 2018 wilayani Ngara Rulenge Stars.
29633019_1808040819235820_780886109_o
Kikosi cha Veterani FC kilichofungwa na Rulenge Stars wakati wa fainali ya Polisi Jamii Cup 2018 wilayani Ngara .
29633155_1808041062569129_533740215_o

29633442_1808041209235781_942876761_o
Hili Kokoto aiseeee uwanjani Kokoto-uwanja wa wilaya ya Ngara mmmmmmmm''Mpira wa fainali huu , Polisi Jamii Cup 2018 wilayani Ngara.

29633745_1808041282569107_830437017_o
Golikipa wa Veteran FC mtumishi wa Benki ya NMB Tawi la Ngara aliibuka Bora wa Mashindano ya Polisi Jamii Cup 2018 wilayani Ngara na kuondoka na zawadi ya fedha 20,000/. koshoto kwake ni Mkuu wa Jeshi wa Polisi wilayani humo Abeid Maige na kulia ni Vedastus Tibaijuka,Katibu Tawala wilaya.
29680648_1808041259235776_572489957_o
Shuja wa mchezo huo ni Elias Jevent  ambaye aliifungia timu yake mabao hayo yote mawili na kumfanya kuibuka mfungaji bora wa mashindano kwa kufikisha mabao 7 na kuondoka na zawadi ya fedha taslimu 20,000/.
Rulenge Stars kwa Kuibuka Bingwa ,amekabidhiwa zawadi yake na Mgeni rasmi Mwenyekiti wa michezo wilaya na Katibu tawala wilaya ya Ngara mkoani Kagera Vedastus Tibaijuka Ng’ombe mnyama ,Kikombe na Mpira mmoja huku Veteran FC wakizawadiwa Mbuzi mnyama na Mpira mmoja wakati washindi wa tatu,Nyakariba FC wakizawadiwa Mbuzi mmoja na Mpira mmoja baada ya kuibuka timu yenye nidhamu.

29635006_1808040602569175_823786704_o
Zawadi ya Mbuzi mnyama za Washindi wa Pili Veteran FC na Nyakariba FC washindi wa 3 wa  Polisi Jamii Cup 2018 wilayani Ngara.
29633804_1808041032569132_1459134422_o
Zawadi ya Bingwa wa Polisi Jamii Cup 2018 wilayani Ngara Rulenge Stars baada ya Kumfunga Veterani FC bao 2-0 katika fainali uwanja wa Kokoto Jana March 25,2018.
29527592_1808041219235780_1724054580_o
Katibu Tawala wilaya ya Ngara mkoani Geita,Vedastus Tibaijuka akimkabidhi Nahodha wa Timu ya Rulenge Stars fimbo iliyozungushiwa kamba kama zawadi ya Ng'ombe mnyama baada ya Rulenge Stars kuibuka mshindi wa Kombe la Polisi Jamii 2018 wilaya ya Ngara mkoani Kagera baada ya kuifunga Veterani FC FC ya Mjini Ngara magoli 2-0.

Rulenge Stars ya mjini Rulenge wameshinda kombe hili kwa mara ya Kwanza toka limeanzishwa na Mkuu wa Polisi wilayani Ngara Abeid Maige Jana March 25,2018 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa uwanja wa Kokoto Mjini Ngara.

Post a Comment

0 Comments