habari


Mwalimu wa Sekondari Kizimbani kwa Kumkashifu Rais Magufuli.

1
Jeshi la Polisi wilayani Ngara mkoani Kagera, limemkamata Mwalimu Deogratius Simon (34), kwa kosa la kumkashifu Rais Dkt John Magufuli kuwa ni dikteta na kwamba anaminya demokrasia kwa kuzuia maandamano na mikutano.

Mwalimu huyo kabila Mhaya ,akifundisha Shule ya Sekondari Nyakisasa,Tarafa ya Rulenge wilayani Ngara aliandika ujumbe wa kumkashifu Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo kati ya tarehe za mwaka 2016 -2018 kupitia ukurasa /akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa facebook iliyosajiriwa kwa jina la Deogratius Simon akitumia simu aina ya tecno y3 yenye laini ya halotel.

Kufuatia tukio hilo,akiielimisha Wananchi kupitia Mashindano ya mpira wa miguu ya Polisi Jamii Cup 2018 yanayoendelea wilayani Ngara yenye kauli mbiu ya ‘’Kataa uhalifu,Fichua wahalifu’’, Mkuu wa Jeshi la Polisi  wilayani humo,Bw. Abeid Maige ameonya baadhi ya watu  wasiopenda amani ya nchi hii wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii  wakivunja shieria  kwa kuahamasisha chuki dhidi ya Serikali.

Bw.Maige amewasisitiza watanzania  kuwa mitandao ya kijamii  isitumike kuchochea uharifu kwa kuacha kutimia lugha ya kichochezi na kuwashawishi watu wengine kuvunja sharia bali itumike kuchochea maendeleo yao.

Mtuhumiwa amesomewa mashitaka yanayomkabili Katika Mahakama ya wilaya ya Ngara March 20, 2018 na amekana ambapo kesi hiyo itatajwa tena Ijumaa hii March 23, 2018.

Post a Comment

0 Comments