habari Mpya


Mtoto Anthony Petro Alipotembelea Radio Kwizera FM - Ngara,Kagera.

Mtoto Anthony Petro akiwasili Ofisi za RADIO KWIZERA –NGARA Mkoani Kagera na ameiambia Redio Kwizera na Wasikilizaji wake kuwa hafurahishwi na maisha wanayoishi kwani hakuna usalama wa kutosha hivyo ni vema wakasaidiwa kutafutiwa eneo lingine kwa ajili ya usalama wao.

Akaunti ya mtoto Anthony Petro Magogwa.

Jina la Account:

Petro, Niyosaba and Paphilius

A/C Na. 01523 46697000

CRDB

Jina la kwanza ni la baba wa mtoto

Jina la pili ni la Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya

Jina la tatu ni la Paroko wao

Imefanyika hivyo ili kudhibiti matumizi ya fedha kwa kuwa watoto bado ni wadogo.

Mtoto Anthony Petro aliyetangulia akiwa na Baba Yake Mzazi, Mzee Petro Magogwa walipowasili Ofisi za Radio Kwizera mjini Ngara.

 Pamoja na Familia hiyo kutoa shukrani kwa wanaojitokeza kuwasaidia ,Afisa Ustawi wa Jamii wilayani Ngara mkoani Kagera Bw. Musa Balagondoza wakati akitoa ufafanuzi wa namna ya kumsaidia mtoto Anthony kupitia kipindi cha Mchakato hapa Redio Kwizera ametoa wito kwa Watu wote walioko ndani na nje ya wilaya ya Ngara kufuata utaratibu wa kupita ofisi ya Ustawi wa Jamii ama Ofisi ya Mkurugenzi kabla ya kuifikia familia ya Petro Magogwa.
 
Alipoulizwa kuhusu baadhi ya makundi ya watu waliojitokeza kuchangisha watu kwa ajili ya mtoto Anthony, Afisa Balagondoza amesema Halmashauri haina taarifa hivyo misaada yote inayotolewa kwa ajili ya mtoto huyo inapaswa kupitia kwenye akaunti maalumu iliyofunguliwa chini ya halmashauri ya wilaya
Pichani Juu na Chini ni Baadhi ya Watumishi wa Kituo cha Radio Kwizera ,Ngara wakimpokea Mtoto Anthony na Baba yake Mzee Petro Magogwa walipokuja kuzungumza na wasikilizaji wa Kituo hicho kupitia kipindi cha Mchakato hapa Redio Kwizera.

Post a Comment

0 Comments