habari Mpya


Mkoa wa Kagera na Agizo kwa Wananchi kuhusu Kilimo na Mkakati wa Lishe Bora.

28795882_1733258423362544_2416318624460394049_n
Baadhi ya Wajumbe wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC0 Kagera.
 
Wananchi Mkoani Kagera waagizwa kila mmoja kulima ekari moja ya zao la chakula na zao la biashara ili kuhakikisha kuwa kila familia inakuwa na chakula chakutosha pia inakuwa na zao la biashara ili kila mwananchi aweze kujiingizia kipato kuondokana na umasikini.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) ambapo aliwaagiza Wakuu wa Wilaya wote wa Mkoa wa Kagera kuhakikisha wanasimamia agizo hilo katika Wilaya zao ili mkoa uzalishe chakula cha kutosha.
 
Mkuu wa Mkoa Kijuu katika kuhakikisha agizo lake linatekelezwa aliwasistiza Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanawasimamia watendaji walioko chini yao kuorodhesha kila mwananchi mwenye uwezo wa kufanya kazi kwenye kaya ili ajulikane na kuonesha shamba lake la zao la chakula na biashara.
 
28783402_1733258453362541_1614606283054220585_n

28783555_1733258306695889_1444911983752767848_n
Mama Anna Tibaijuka-kushoto,Mbunge wa Muleba Kusini CCM.
 
Mkoa huu hautakiwi kuwa na umasikini kwasababu una hali nzuri ya hewa, misimu miwili ya mvua, una ardhi yenye rutuba na ya kutosha kwa kilimo. Hakuna haja ya vijana kukimbili katika shughuli za bodaboda wakati kuna fursa ya kilimo, lazima tulisimamie hili kwa nguvu zote.” Alisistiza Mhe. Kijuu.
 
Aidha, Mhe. Kijuu alibainisha kuwa Mkoa wa Kagera kuna matunda mengi lakini wananchi hawana tabia ya kula matunda na kupelekea watoto wengi kuwa na utapiamlo na udumavu ambapo alisisitiza juu ya Kampeini yake ya kupanda miche ya miti ya matunda na kila kaya kupanda miti mitano ya matunda na kuitunza.
 
28870061_1733258286695891_3680650023381977539_n
Wajumbe wakifatilia mkutano huo.
 
Mwaka 2017/2018 Mkoa wa Kagera umeweka lengo la kuzalisha tani 3,876,000 za mazao ya nafaka hadi kufikia mwezi Februari, 2018 mkoa tayari umezalisha tani 2,551,000 sawa na asilimia (65%) ya lengo la uzalishaji wa mazao ya nafaka.
 
Katika hatua nyingine kikao hicho cha Ushauri cha Mkoa wa Kagera kimeridhia na kuidhinisha kiasi cha shilingi 387,774,822,000/= kwa ajili ya miradi ya maendeleo na matumizi ya kawaida kwa mwaka wa fedha 2018/2018 ambapo matumizi ya kawaida zitatumika shilingi 294,664,409,000/=
 
Mishahara shilingi 274,351,117,000/= na matumizi mengineyo shilingi 20,313,292,000/=, shilingi 66,794,398,000/= ni kwaajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo, na shilingi 17,316,015,000/= zitakusanywa kutoka vyanzo mbalimbali vya ndani ya mkoa kwajili ya kugharimia shughuli za maendeleo na za kawaida.
 
Na: Sylvester Raphael

Post a Comment

0 Comments