habari


Mamlaka zinazohusika haya Matawi ya Mti kwenye Kibao cha Alama ya Kivuko cha Watembea kwa Miguu kulikoni?

Pichani Juu na Chini ni muonekano wa Kibao cha Alama Sahihi za Usalama Barabarani chenye kuonesha Alama ya kuvuka kwa  watembea kwa miguu kikiwa kimefunikwa na matawi ya mti katika barabara kuu ya Ngara kuelekea nchini Burundi mkoani Kagera eneo la Benki ya CRDB Tawi la Ngara na Kanisa Katoliki ambapo bila ya kuonekana madereva wanaweza kusababisha ajali wakitakiwa kupunguza mwendo kasi kwenye barabara hiyo.


Mamlaka zinazohusika wahini kukata matawi hayo jamani  ili madereva waone alama ya kibao hicho kwa urahisi kuepuka kutokea madhara yakiwemo ya watu kupoteza maisha sababu za uzembe.USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE.

Post a Comment