habari Mpya


Liverpool dhidi ya Manchester City katika robo fainali ya Champions League.

Jana Ijumaa March 16,2018, ratiba ya robo fainali ya Champions League 2017/2018 imetoka na Juventus wameangukia tena mikononi mwa Real Madrid, hii ni nafasi nyingine tena kwa wababe hawa wa Italia kulipa kisasi kwa Real Madrid.

Liverpool dhidi ya Manchester City katika robo fainali ya Champions League, huu ni mchezo ambao baada ya droo tu kutangazwa tayari umeshakuwa gumzo sana kutokana na viwango vya timu hizi mbili.

Bayern Munich wanaonekana kuwa na bahati, kwani timu zote zilikuwa zikiomba kupewa Sevilla katika hatua hii kwani ndio timu inaonekana dhaifu na Bayern Munich wamefanikiwa kuipata bahati hiyo.

FC Barcelona nao, kama ilivyo kwa Sevilla, As Roma ni timu nyingine inaonekana dhaifu na Fc Barcelona wamepata bahati kukutana na Roma, michezo hii inatarajia kupigwa kati ya tarehe 3 hadi 11 April,2018.

HAPA CHINI NI RATIBA KAMILI.

Post a Comment

0 Comments