habari Mpya


Kahawa ya Bw.Odasi Mathayo kijiji cha Buhororo wilaya ya Ngara mkoani Kagera.

28279103_1844257175647668_5286161338040147512_n
Mmea wa Kahawa ukiwa Shambani katika kijiji cha Buhororo wilaya ya Ngara mkoani Kagera Bw.Odasi Mathayo.

  Sekta  ya  Kilimo  ni  mhimili  wa  uchumi  wa  Tanzania  na  imekuwa  ikichangia  Pato la  mkulima mmoja mmoja, kaya na Taifa kwa ujumla pia ni tegemeo la mapato ya fedha za ndani na za nje ya nchi.

Sekta hii imeajiri zaidi ya asilimia 70 ya idadi ya watu wote nchini na kuzalisha mazao ya chakula na biashara. Mazao makuu ya chakula ya aina ya wanga yanayozalishwa ni pamoja na mahindi, muhogo, mpunga na mtama.

Mazao mengine ni ndizi, viazi vitamu na viazi mviringo,  ngano,  ulezi  na  uwele.  Mazao  ya  mikunde  ni  pamoja  na  maharage,  kunde, mbaazi, choroko na njegere. Mazao yote hayo ndiyo yanayochangia Taifa kujitosheleza kwa  chakula  kwa  zaidi  ya  asilimia  100.

 Mazao makuu  ya  biashara  ni  korosho,  miwa  kwa  ajili  ya sukari, pamba, mkonge, tumbaku, pareto, kahawa na chai.

Mazao mengine ni ya bustani na mbegu za mafuta.
28055791_1844257268980992_7880619478752155126_n
Mkulima wa zao la Kahawa katika kijiji cha Buhororo wilaya ya Ngara mkoani Kagera Bw.Odasi Mathayo, akifanya uchunguzi na kuondoa vikonyo kwenye matawi ya zao hilo analotegemea kuvuna mwezi Mei mwaka huu kama alivyokutwa shambani na mpiga picha Februari 20, 2018.
27973912_1844257202314332_7352976256553417018_n

28059049_1844257138981005_6443938451378444472_n

28276292_1844257312314321_2764664304644002797_n

Post a Comment

0 Comments