Kamanda wa Jeshi
la Polisi mkoani Kigoma ACP Martin Othieno ametoa muda huo March 21, 2018
kufuatia kuongezeka kwa matukio ya uhalifu yanayodaiwa kufanywa na wakimbizi
kutoka nchini Burundi ambao wanamiliki silaha kinyume cha sheria.
Jeshi la Polisi
mkoani Kigoma limetoa mwezi mmoja kwa raia wa Burundi waishio katika kambi za Wakimbizi
mkoani humo kusalimisha silaha kabla ya kufanyika kwa msako mkubwa baada ya
kubainika wengi wao kumiliki silaha hizo kinyume cha sheria.
Kamanda wa
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma ACP Martin Othieno ametoa muda huo leo kufuatia
kuongezeka kwa matukio ya uhalifu yanayodaiwa kufanywa na wakimbizi kutoka
nchini Burundi ambao wanamiliki silaha kinyume cha sheria.
Akizungumzia
tukio la hivi karibuni Kamanda Othieno amesema polisi bado inawasaka watu
watatu kati ya watano wanaodaiwa kuwa majambazi kufuatia kutoroka baada ya
majibishano ya risasi katika eneo la pori la Makere Wilayani Kasulu ambapo
majambazi wawili walifariki papo hapo.
ACP Othieno
amewataja waliokufa kuwa ni washirika wawili, raia wa Tanzania mkazi wa Kasulu
Nobert Andrew na Raia wa Burundi Bukuru Steven mkazi wa kambi ya Nyarugusu
waliokuwa wakimiliki bundiki AK47 na risasi 41.
|
0 Comments