habari Mpya


Baadhi ya Maduka yafungwa Kigoma Ujiji kisa Tozo ya shilingi 50,000.

Baadhi ya maduka yaliyofungwa na Manispaa ya Kigoma Ujiji kutokana na kugomea tozo ya shilingi 50,000.

Baadhi ya maduka yaliyofungwa na Manispaa ya Kigoma Ujiji kutokana na kugomea tozo ya shilingi 50,000.

Manispaa ya Kigoma Ujiji imeyafunga maduka katika Soko Kuu la Mwanga kutokana na mgogoro wa tozo jipya ya ushuru la shilingi 50,000 kutoka 15,000, uliodumu kwa muda sasa.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa soko hilo, Raymond Ndabhiyegese amesema, walipata taarifa ya kufungiwa maduka yao takribani mwezi mmoja uliopita kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa, Dkt. John Shauri.

Kaimu mkurugenzi huyo inadaiwa aliwaeleza wafanyabiashara hao kuwa atafungia kila duka ambalo litakaidi kulipa tozo hiyo.

Post a Comment

0 Comments