habari


Askofu Severine Niwemugizi Aongoza Ibada ya Misa ya kubariki Mafuta katika Kanisa la Mt Fransisko wa Asizi mjini Ngara.

Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge,Ngara, Wilaya ya Ngara, mkoani Kagera, Severine Niwemugizi akichanganya marashi kwenye mafuta matakatifu ambayo ni mafuta ya KRISMA, Mafuta ya wagonjwa na mafuta ya wakatekumeni wakati wa Ibada ya Misa ya kubariki mafuta iliyoadhimishwa Jana March 22,2018 katika kanisa la Mt Fransisko wa Asizi mjini Ngara .

Hapa Mapadri wakati wakirudia ahadi zao.

Mafuta ya krisma yanatumika kuwapaka wachungaji wa kanisa katoliki katika viganja vyao, pamoja na ubatizo.

Mafuta ya wagonjwa hutumika kwa ajili ya mpako wa wagonjwa.

Mafuta ya wakatekumeni hutumika kwa ajili ya wale wanafunzi wa dini wanaojifunza kwa ajili ya ubatizo.

Mapadre wa Jimbo la Rulenge Ngara mkoani Kagera wakiwa kwenye Ibada ya Misa ya kubariki mafuta iliyoadhimishwa Jana March 22,2018 katika kanisa la Mt Fransisko wa Asizi mjini Ngara .

Post a Comment

0 Comments