habari Mpya


Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera wilayani Ngara Kukagua Ujenzi wa Vituo vya Afya.

27845992_1751887234851179_979102428_o
Picha ya Pamoja ya Watumishi wa Shule ya Sekondari Murusagamba na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu (suti ya kijivu) wakati wa ziara ya siku moja wilayani Ngara February 5,2018 Kukagua ujenzi wa miradi mitatu ya Kituo vya Afya Murusagamba , Mabawe  na Mabweni ya Sekondari ya Murusagamba.

Kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ngara,Luten Kanali Michael Mtenjele.

27786041_1751887321517837_598740273_o
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu amefanya ziara ya siku moja wilayani Ngara February 5,2018 Kukagua ujenzi wa miradi mitatu ya Kituo vya Afya Murusagamba kinachofanyiwa upanuzi kwa kujengwa wodi na nyumba za watumishi ambapo mpaka kukamilika zitatumika Sh Milioni 400, Kituo cha Afya Mabawe ambacho nacho kinafanyiwa upanuzi wa majengo kikitengewa Sh Milioni 400 na Mabweni ya Sekondari ya Murusagamba ambayo hata Mkuu wa mkoa alikataa kuyazindua na kuagiza yafanyiwe marekebisho kutokana na kukutwa na mapungufu.
27836532_1751887281517841_252897399_o

27747244_1751887231517846_478984786_o
Wananchi wa Mabawe wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu aliyefika Kituo cha Afya Mabawe kukagua ujenzi wa Kituo hicho kinachofanyiwa upanuzi wa majengo ili kuboresha huduma za afya.

Post a Comment

0 Comments