habari Mpya


Siku ya Sheria na Mafanikio yaliyofikiwa na Mahakama wilayani Ngara mkoani Kagera 2017.

IMG_20180201_123906
Mahakama ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera imesikiliza  mashauri 793 na kuyatatuliwa  kisheria baada ya kufikishwa mahakamani hapo kwa mwaka 2017 ambapo  mashauri 608 yalihusiana na makosa ya  jinai na 185 yalikuwa ya madai.
 
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Ngara Bw Joseph Luambano amesema hayo baada ya kutembelea gereza la wilaya ya Ngara na kuzungumza na wafungwa pamoja na  watendaji wa gereza hilo.
 

 Akizungumza katika siku ya maadhimisho ya siku ya  mahakama ambayo hufanyka februari  mos kila mwaka  kwa wilaya ya Ngara maadhimisho hayo yamefanyika katika  ukumbi wa mkuu wa wilaya hiyo  ambapo maadhimisho hayo yamewashirikisha  viongozi wa serikali , viongozi wadini mbalimbali na wadau washeria.
 

IMG_20180131_103859
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera Joseph Luambano.
 
Bw. Luambano amesema wilaya ya Ngara inazo mahakama  13 za mwanzo ambazo kwa mwaka 2017 zimesikiliza  mashauri 779 kati yake 595 ni mashauri ya jinai na 184 ni mashauri ya madai ambapo mahakama sita hazifanyi kazi kutokana na changamoto za miundombinu kiutendaji.
 
“Kwakiasi kikubwa mahakama zetu zimejitahidi kufanyakazi kwaufanisi zaidi katika wilaya yetu ya Ngara tuna jumla ya mahakama 13 za mwanzo na kwa mwaka 2017 mahakama hizo zimesikiliza mashauri 779ambapo kati ya hayo masahauri 595 ni mashauri ya jinai na 184 ni mashauri ya madai “alisema Luambano.
 
IMG_20180201_102921
Wa kwanza kutoka kushoto ni Gidion Bagwobweki ambaye ni Afisa Tawala wa Mahakama wilaya ya Ngara anaye fuata ni kuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera Luteni Kanali Michael Mangwela Mtenjele na watatu ni Hakimu mkazi mfawidhi wa mahaqkama ya wilaya Joseph Luambano. katika maadhimisho ya siku ya mahakama.
 
IMG_20180201_102308

IMG_20180201_103322
Wadau mbalimbali katika Muonekano wakati wa maadhimisho hayo huku  aliyesimama mwenye  suti nyeusi ni Mchungaji wa kanisa la Anglikana Palishi ya Ngara mkoani Kagera, Diocess ya Kagera Mch .Amoni Kanoni Nzikombankunda akitoa maombezi katika ufunguzi wa maadhimisho hayo.
 
IMG_20180201_123919
Picha ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa mahakama na serikali na viongozi wa dini walio hudhuliria maadhimisho hayo wakiwemo wadau wa sheria na hii ni baada ya kuhitimisha maadhimisho hayo  wakapata picha ya pamoja kama sehemu ya kumbukumbu.
 
IMG_20180201_103238
Bi. Agnes Lulu Malimbo  Kalani wa Mahakama ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera  ambaye pia alikuwa miongoni mwa waliohudhuria katika maadhimisho hayo ya siku ya mahakama.
 
Itakumbukwa kuwa pia February mosi ilikuwa kilele cha siku ya sheria ambapo wananchi na wadau mbalimbali wa sheria wilayani Ngara wamesema serikali haina budi kuandaa vipeperushi na kuvisambaza kwenye maeneo mbalimbali  kutambua maana ya kauli mbiu  ya wiki ya sheria, ambapo kwa mwaka huu kauli mbiu ni “Matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa haki kwa wakati na kwa kuzingatia maadili”.

Post a Comment

0 Comments