habari Mpya


Pendekezo la Pius Ngeze kuifuta Mamlaka ya Mji mdogo wa Rulenge wilayani Ngara.

1
Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera kwa kushaurisha Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI imeshauriwa kuifuta mamlaka ya mji mdogo wa Rulenge wilayani humo kwa madai imeshindwa kujiendesha.

Ushauri huo umetolewa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoani Kagera na mbunge mstaafu wa jimbo la Ngara Pius Ngeze (Pichani ) katika barua aliyomwandikia Mwenyekiti wa halmashauri ya Ngara, Erick Nkilamachumu.


Baada ya barua hiyo iliandikwa Desemba 12,2017 kisha kusambaa kwa watu mbalimbali ndani na nje ya wilaya ya Ngara ambapo wananchi wamemlalamikia Pius Ngeze kwa kupinga maendeleo ya mamlaka yao.
4
Wakizungumza February 7 mchana katika mkutano wa hadhara wa kata ya Rulenge, baadhi ya wananchi wamewataka viongozi kubainisha vipengele vilivyopendekezwa na Ngeze vinavyobainisha kuifuta mamlaka ya mji mdogo wa Rulenge.


Katika mkutano huo Jamadali Ruguge na Simon Nyabenda wamemtaka Mtendaji wa Halamshauri kuwaeleza wananchi kama malaka hiyo inayo hati ya utambulisho na kutoa taarifa ya mapato na matumizi pamoja na changamoto zilizopo kiutendaji.


Katika barua hiyo Ngeze alifafanua kuwa vijiji vitatu vya Munjebwe Rulenge na Muyenzi viliwekwa kuwa ndani ya Mamlaka lakini halmashauri ya wilaya ya Ngara imeshindwa kuboresha miundombinu ya barabara maji na umeme.


Amesema watendaji wa mammlaka wanashindwa kuendesha vikao kwa kukosa posho za wajumbe licha ya kusanywa mapato yanayopelekwa halmashauri ya wilaya na hakuna mrejesho wa kuendeleza miradi ya wananchi wa Rulenge.

3
Barua hiyo ilitaja huduma zinazotakiwa kuwa zimeboreshwa katika mamlaka hiyo iliyoanzishwa mwaka 2015 baada ya kupendekezwa na Mbunge mstaafu wa jimbo la Ngara Deogratias Ntukamazina ni ujenzi wa kituo cha Afya, Soko , shule nk.


Mamlaka ya mji mdogo wa Rulenge yenye vitongoji 17 vyenye wakazi 17,826 walioko kwenye kata moja ya Rulenge , wananchi hao wanalalamikia pia Pius Ngeze kwa kuhodhi ardhi kubwa bila kuiendeleza wakikosa huduma za kijamii.


Ngeze alipotafutwa kueleza malengo ya kuandika barua hiyo amekiri na kudai kuwa Halmashauri haina budi kuifuta na kubaki serikali za vijiji ambapo viongozi wataweza kujiwekea mipango ya maendeleo bila kuwa tegemezi.


“Mamlaka zote duniani haziwezi kujiendesha bila fedha za kutekeleza miradi yake ambapo mamlaka ya mji wa Rulenge ni tegemezi toka halmashauri ya wilaya na mkurugenzi mtendaji ameshindwa kuisimamia” Amesema Ngeze.


Aidha amesema ardhi anayolalamikiwa kuimiliki kinyume na utaratibu ni mali yake na wanafamilia ambayo aliioomba serikali ya kijiji cha Rulenge mwaka 1984 baada ya kuhamia kijiji hicho akitokea kijiji cha Muganza wilayani humo.


Amesema baada ya kuibuka madai ya ardhi hiyo kutoka kwaa baadhi ya watu waliounda kikundi cha madai ya ardhi na kufunguliwa kesi mahakama ya wilaya ya Chato na kuwashinda baada ya kuonyesha vielelezo na nyaraka zilizotakiwa.
5
Hata hivyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara, Erick Nkilamachumu ( pichani ) amesema barua aliyoandikiwa na Ngeze akipendekeza kuifuta Mamlaka ya Rulenge imepokelewa lakini hadi kukaa vikao rasmi kupita ofisi ya Rais TAMISEMI.


Amewataka wananchi kuvuta subira wakizubiria baadhi ya kero kama migogoro ya ardhi kutatatuliwa na Waziri mwenye dhamana Wiliam Lukuvi anayetarajia kufanya ziara wilayani Ngara muda mfupi ujao.

Post a Comment

0 Comments