habari Mpya


Yanga SC Yaanza na Ushindi wa 2-1 Mlandege –Mapinduzi Cup 2018.

mahadhi
Yanga SC imeanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi 2017/2018 baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Mlandege katika mchezo wa Kundi B Uwanja wa Amaan, Zanzibar usiku wa Jana January 2, 2018.
 
Shujaa wa Yanga jana alikuwa ni kiungo aliyetumika kama mshambuliaji , Juma Mahadhi aliyefunga mabao yote mawili kipindi cha kwanza katika dakika ya 6 na dakika ya 36.
 
Beki wa Yanga, Andrew Vincent Chikupe ‘Dante’ alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 88 pamoja na beki wa mshambuliaji wa Mlandege, Omar Makame baada ya kugombana. 
 
Katika mchezo uliotangulia leo wa Kundi B, Singida United imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Zimamoto hapo hapo Amaan. 
 
Mabao ya Singida yamefungwa na Deus Kaseke dakika ya saba, Dany Usengimana dakika ya 21 na Kigi Makasi dakika ya 81, wakati ya Zimamoto yamefungwa na Ibrahim Hamad Ahmada ‘Hilika’ katika daika ya 39 na 84.
2018%2BMAPINDUZI%2BCUP%2BNEW%2BDRAFT%2BFIXTURE....
Azam FC watarudi tena uwanjani Januari 3, 2018 kumenyana na Jamhuri SC Saa 10:30, baadaye URA Januari 5, 2018 Saa 10:30, kabla ya kukutana na Simba SC Januari 6 Saa 2:15 usiku kukamilisha mechi  zake za Kundi A.
 
Simba SC watarudi uwanjani Januari 4 kumenyana na Jamhuri Saa 2:15 usiku, kabla ya kukutana na Azam FC Januari 6 na kuhitimisha mechi zake za Kundi A kwa kumenyana na URA Januari 8, 2018 Saa 10:30 jioni.
 
Yanga SC wao watarudi uwanjani  Januari 4 Saa 10:30 jioni kumenyana na JKU, kabla ya kupepetana na Taifa ya Jan’gombe  Saa 2:15 usiku Januari 5, Zimamoto Saa 2:15 usiku Januari 7 na kukamilisha mechi zake za Kundi B Januari 8 kwa kumenyana na Singida United.

Post a Comment

0 Comments