habari Mpya


Yanga SC na URA katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi Jumatano January 10,2018.

Wekundu wa Msimbazi Simba SC wametolewa kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar baada ya kuchapwa bao 1-0 na URA ya Uganda ambayo ni timu mwalikwa katika mashindano hayo.

Simba inayaaga mashindano hayo ya mwaka huu kutokana na kumaliza katika nafasi ya tatu ya kundi A, ikiwa imeambulia pointi nne pekee katika michezo minne iliyocheza kwenye kundi lake, huku URA wakichukua uongozi wa kundi kwa kufikisha pointi 10 wakifuatiwa na Azam FC nafasi ya pili wenye pointi 9.
URA na Azam sasa uwanaunga na Timu za kundi B kati ya Singida United na Yanga SC kucheza hatua ya nusu fainali. 

Yanga SC itakutana na URA ya Uganda katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi Jumatano January 10,2018 Uwanja wa Amaan, Zanzibar wakati Singida United itacheza na Azam FC.

Hiyo ni baada ya Yanga kutoka sare ya 1-1 na Singida United katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi usiku huu Uwanja wa Amaan.

Nusu Fainali ya kwanza itakuwa kati ya Yanga na URA Saa 10:30 jioni na saa 2:15 usiku Singida United na Azam zitachukua nafasi kwa mujibu wa ratiba kama hakutakuwa na mabadiliko.

Post a Comment

0 Comments