habari Mpya


URA na Azam FC za Kundi A katika Fainali Mapinduzi Cup- January 13,2018.

Timu ya Azam FC imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Mapinduzi 2018 baada ya ushindi wa bao 1-0 usiku wa jana January 10, 2018  dhidi ya Singida United Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Bao hilo pekee la  Shaaban Iddi Chilunga aliyefunga dakika ya 78 kwa shuti kali lililompita kama mshale kipa wa Singida, Peter Manyika baada ya kumtoka beki Michael Rusheshangoga upande wa kushoto.

Azam  FC  ambao ndiyo Mabingwa watetezi, sasa watakutana na URA ya Uganda katika fainali Jumamosi January 13,2018 katika Uwanja wa Amaan.
URA na Azam FC zimetokea Kundi A ambako ziliwapiku vigogo, Simba SC ya Dar es Salam walioshindwa kuingia hatua ya mtoano.

Ikumbukwe katika mchezo uliotangulia, URA iliwatupa nje Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.

Ni mara ya tatu mfululizo Yanga SC kupoteza mechi ya nusu fainali na kuaga mashindano ya Mapinduzi kwani mwaka 2016 na 2017 pia ilipoteza nusu fainali zake na kushia kuisikia fainali ya mapinduzi kwa muda mrefu.

Yanga SC wamepoteza nusu fainali kwa mara ya pili mfululizo dhidi URA na mara zote wakitolewa kwa mikwaju ya penati, mwaka 2016 walitupwa nje ya mashindano kwa penati 4-3 baada ya sare ya kufungana 1-1.

Post a Comment

0 Comments