habari Mpya


Ujumbe maalum wa Rais Museveni kwa Rais Magufuli.

Rais Magufuli akipokea barua kutoka kwa rais Museveni kupitia mjumbe wake maalum.

Rais John Magufuli leo, Januari, 4 amepokea barua kutoka kwa rais  mwenza wa Uganda, Yoweri Museveni iliyowasilishwa na mjumbe maalum Sam Kutesa ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda.

Pamoja na kupokea barua hiyo, rais Magufuli amefanya mazungumzo waziri Kutesa, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya mazungumzo hayo, Sam Kutesa amesema, rais Museveni amemtumia rais Magufuli na watanzania wote salamu za heri ya mwaka mpya pamoja na  kuzungumzia masuala yanayohusu uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda.

Sam Kutesa amesema Uganda inafurahishwa na kuridhishwa na uhusiano uliopo kati ya nchi hizi mbili pamoja na ushirikiano mzuri na wa kindugu uliopo kati yake na Tanzania.

“Tumezungumza namna tutakavyoimarisha na kukuza zaidi uhusiano wetu katika maeneo mbalimbali, kama unavyojua kuna miradi ya maendeleo ya ushirikiano ukiwemo mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga hapa Tanzania, na miradi mingine na masuala mbalimbali ya ushirikiano” amesema Sam Kutesa.

Post a Comment

0 Comments