habari Mpya


Treni yashika Moto Afrika Kusini baada ya Kugonga Lori.

_99462885_er24
Treni ya kubeba abiria imeshika moto baada ya kugongana na lori nchini Afrika Kusini.
 
Maafisa wa Afrika Kusini wasema jumla ya watu 12 wamefariki dunia na wengine 268 kujeruhiwa.

Ukanda wa video uliosambazwa kwenye mitandao umeonesha namna behewa moja la treni hiyo likiwaka moja huku pembeni kukiwa na gari lililopondwa pamoja na lori lililopinduka.
_99462892_traincollision2-2
Abiria ambao wameokolewa kwenye treni hiyo walionekana kuwa pembeni na mizigo yao wakiwa wamepigwa butwaa.
 
Ajali hiyo ilitokea karibu na mji wa Kroonstad katika jimbo la Free State baada ya lori kushindwa kusimama katika makutano ya barabara na reli.
 
Polisi wamenukuliwa wakisema takiribani abiria 850 wameondolewa kutoka kwenye treni hiyo wakiwa salama.

Post a Comment

0 Comments