habari Mpya


Tanesco wawatoa hofu Watumiaji wa Umeme Nchini.

Mitambo katika Kituo cha uzalishaji na usambazaji umeme Kinyerezi.

Shirika la Umeme nchini (Tanesco) limesema hali ya uzalishaji na usambazaji wa umeme nchini ipo katika kiwango kizuri baada ya kuanza kuzalisha umeme katika mitambo miwili ya Kinyelezi.

Hali hiyo imewekwa bayana leo, Jumatano na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dkt. Tito Mwinuka alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Dkt. Mwinuka amesema, mpaka sasa katika maeneo mengi hali ya upatikanaji umeme imeimarika na itaendelea kuboreka kutokana jitihada kubwa za mafundi katika kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme nchini.

Suala la kukatika umeme na hata kuwepo na umeme hafifu lilizua taharuki na kusababisha kero kadhaa kwa wananchi wanaotumia huduma hiyo na hivyo kupelekea TANESCO pamoja na Waziri wa Nishati, Dkt. Merdard Kalemani  kutangaza uwepo wa matangenezo katika kituo kikuu cha usambazaji umeme cha Kinyerezi I na II.

Hata hivyo waziri Merdard Desemba mwaka jana aliaahidi kuwa tatizo hilo litamalizika katikati ya mwezi Disemba 15, 2017.

Post a Comment

0 Comments