habari Mpya


Taarifa ya Redio Kwizera Kuhusu Waandishi wa Habari Kukamatwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Uongozi wa redio Kwizera Fm umetoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, na kuenea katika mitandao ya kijamii inayomuhusisha mmoja wa waandishi wake anayetuhumiwa kujifanya afisa usalama wa Taifa na kujipatia fedha isivyo halali kutoka kwa mganga wa jadi.

Mkurugenzi wa Radio Kwizera, Padre Damas Missanga amesema taasisi inamtambua mtuhumiwa huyo Bw. Saimoni Dionizi kama mwandishi wa kujitegemea anayeripotia Radio Kwizera kutoka Kahama lakini tuhuma hizo haziihusu taasisi na wala hakutumwa kufanya hivyo.

Padre Missanga ameeleza kwamba Radio Kwizera, kama chombo cha habari kitaendelea kujikita katika maadili ya uandishi wa habari wakati wote, kutoa huduma kwa jamii kwa kuzingatia haki, weledi na sheria za nchi na hivyo  inaomba radhi kwa wadau na wasikilizaji wote waliopata usumbufu kutokana na taarifa hiyo.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari inaeleza kuwa waandishi wa habari watano wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamefikishwa mahakamani kwa makosa ya kujifanya maafisa usalama wa taifa na kujipatia shilingi Milioni 1 kutoka kwa Jane Mbeshi mkazi wa kitongoji cha Ng’wande kata ya Mwaluguli ambaye ni  mganga wa jadi.

Waandishi hao ni Paul Kayanda wa gazeti la Uhuru, Raymond Mihayo- Habarileo, Shaban Njia-Jamboleo, Simon Dioniz- Radio Kwizera na George Maziku ambaye hajulikani anaandikia chombo gani.

HAPA CHINI ISOME TAARIFA KAMILI.Post a Comment

0 Comments