habari Mpya


Simba yaitandika Jamhuri 3-1 Kombe la Mapinduzi 2018.

20180104_234825-1024x671
Simba SC Jana January 4, 2018 wamepata ushindi wao wa kwanza dhidi ya Jamhuri katika mashindano yo Kombe la Mapinduzi 2018 baada ya kutoka sare mchezo wao wa kwanza.
 
Iliwachukua Simba SC dakika nne tu kuandika goli la kwanza kupitia John Bocco na baada ya nusu saa Simba iliandika goli la pili kupitia Moses Kitandu katika dakika ya 33.
Akiichezea Simba SC kwa mara ya kwanza tangu alipossajiliwa kutoka klabu ya Lipuli mwezi uliopita, beki mshambuliaji Asante Kwasi alihitimisha karamu ya magoli kwa Simba SC kwa kuweka kimiani goli safi katika dakika ya 58.
 
Dakika mbili kabla ya mchezo kuisha, Moses Nassoro aliwapatia Jamhuri goli la kufutia machozi kwa shuti kali la mpira wa adhabu.
 
Simba SC imefikisha pointi nne baada ya kucheza mechi mbili, mchezo wa kwanza walilazimishwa sare ya kufungana goli 1-1 na Mwenge. 
 
Pointi nne zinawafanya wapae hadi nafasi ya pili nyuma ya Azam FC ambao wana pointi sita wakiwa wamecheza mechi mbili pili mbili.
 
Kwasi ndio mambo yake kufunga, akiwa na Lipuli tayari alishafunga magoli matano kwenye ligi kuu ya Tanzania bara akiwa ndiye beki mwenye magoli mengi zaidi hadi sasa. Magoli hayo (matano) yanamfanya kuwa nyuma kwa magoli matatu dhidi ya mchezaji anaeongoza kwa magoli hadi sasa ambaye ni Emanuel Okwi wa Simba SC.
 
Kwa matokeo hayo, Jamhuri na Mwenge zinaaga mashindano hayo huku kipute cha Kundi A kikibaki baina ya bingwa mtetezi Azam FC, Simba na URA ya Uganda ambapo kigogo mmoja inabidi atoke na kupisha timu mbili zitakazosonga nusu fainali.

Post a Comment

0 Comments