habari Mpya


Simba SC Yaifumua Majimaji FC raundi ya kwanza Ligi Kuu 2017/2018.

IMG_0560
Kikosi cha Simba SC.
Simba SC kwa mara nyingine tena wamefanikiwa kujizolea Point 3 baada ya kuifunga Majimaji FC magoli 4-0, magoli ya Simba SC yakifungwa na John Bocco aliyefunga mawili dakika ya 16, 26 na Emmanuel Okwi aliyefunga magoli mawili pia dakika ya 52 na 68.
IMG-20180128-WA0103-640x425

IMG_0545
Kikosi cha Majimaji FC.
 
Ushindi huo umeifanya Simba SC kufikisha jumla ya Point 35 na kuendelea kuongoza Ligi kwa kufikisha Jumla ya Point 35 wakifuatia na Azam FC wenye Point 30 huku Singida United baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons wamesogea nafasi ya nne kwa kufikisha Point 27.
 
27336736_2005770306363014_1976777848989275611_n
Mshambuliaji wa Simba SC,John Bocco  Jana  Januari 28, 2018 amefunga magoli mawili dhidi ya Majimaji FC na kufikisha magoli saba (7) kwenye msimu huu wa Ligi 2017/2018 ambapo raundi ya kwanza imemalizika baada ya kila timu kucheza mechi 15.
 
Katika mechi za hivi karibuni Bocco amefunga magoli muhimu ambayo yaliamua baadhi ya mechi, (Tanzania Prisons 0-1 Simba SC, Ndanda FC 0-2 Simba SC, Simba SC 4-0 Majimaji FC ) Bocco amefunga mabao matano katika mechi hizo ambazo Simba ilifunga magoli saba.
 
Mshambuliaji huyo wa Simba SC ameungana na Obrey Chirwa (Yanga SC) Mohamed Rashidi (Tanzania Prisons) na Habib Kiombo (Mbao FC) wote wakiwa wamefunga magoli saba.
 
27067072_2005769656363079_2099284510323886263_n

Post a Comment

0 Comments