habari Mpya


Picha -Hospitali ya Rubya Yapokea Vifaa Tiba Kuboresha Huduma za Matibabu.

Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba mkoani Kagera Methodius Kilaini akisaini kitabu cha wageni mbele ya mganga mkuu wa Hospitali ya Rubya mkoani humo George Kasibante (kulia) baada ya yeye na wafadhili wa hospitali hiyo kutoka nchini Uholanzi kufika hivi karibuni kukabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya Sh 232.32 Milioni kuboresha huduma za matibabu na kupunguza vifo kwa wajawazito na watoto.


Mganga mkuu wa Hospitali ya Rubya Dr George Kasibante wilayani Muleba mkoani Kagera (kulia) akitoa maelezo kwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba mkoani Kagera, Methodius Kilaini na Wajumbe wa Bodi ya Afya ya Hospitali hiyo baada ya kupokea pikipiki mbili zilizotolewa na wafadhili kutoka nchini Uholanzi ikiwa ni sehemu ya vifaa tiba vilivyotolewa na wafadhili hao kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa yasiyotibika ili kuwaongezea siku zao za kuishi.

Post a Comment

0 Comments