habari Mpya


Orodha ya Mikoa iliyofanya Vizuri Vitambulisho vya Taifa 2017.

Kaimu  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Andrew Massawe, ameitaja mikoa ya Mara, Arusha, Iringa, Geita, Lindi, Simiyu, Mbeya na Songwe kuwa inayoongoza katika kuwasajili wananchi kupata vitambulisho vya Taifa kwa Mwaka 2017/2018.


Huku mikoa mingine ikiwa nyuma kiusajili kulinganisha na malengo waliyowekewa.

Akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa zoezi la usajili kwa mkoa wa Ruvuma lililofanyika mjini -Songea, Massawe alimuomba Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, kusaidia kuweka msukumo kwa viongozi na wananchi kwenye mikoa ambayo haifanyi vizuri, ili iongeze kasi ya usajili kwa lengo la kukamilisha usajili kwenye mikoa yao kwa muda uliopangwa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme, alimhakikishia Nchemba mkoa wake uko tayari kusimamia na kuhakikisha wananchi wote wenye sifa wanasajiliwa na kupata vitambulisho katika muda uliopangwa na hatamvumilia mtu yeyote ambaye atakuwa kikwazo katika utekelezaji wa zoezi.

Mkoa wa Ruvuma wenye wilaya 5 unakisiwa utawasajili zaidi ya wananchi 900,000 katika zoezi lililopangwa kumalizika ndani ya miezi mitatu. Mikoa mingine inayoendelea na usajili ni Iringa, Mbeya, Njombe, Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga, Geita, Simiyu, Mara, Songwe, Lindi na Mtwara.

Post a Comment

0 Comments