habari Mpya


Onyo la Serikali kuhusu Shule zinazonyanyasa Wanafunzi wasiofanya Vizuri.

shool_1515766592-1600x705
Jengo la Shule Binafsi.
 
Wizara ya Elimu nchini imezionya shule zisizo za kiserikali zinazofukuza au kuwahamisha wanafunzi kwa kigezo cha kutofikia wastani wa ufauli wa shule kuacha kufanya hivyo mara moja.
Aidha kupitia waraka wa Elimu Namba 7 wa Mwaka 2004, wizara hiyo pia imewataka wazazi ambao watoto wao walikutana na adha hiyo kuwarejesha katika shule hizo na shule itakayokaidi itachukuliwa hatua za kisheria kwa kufutiwa leseni ya usajili au kufungiwa kabisa.
 
Wanafunzi ambao wamedaiwa kukutana na sakata hilo ni pamoja na wale wanaofanya mitihani ya darasa la Nne na Kidato cha pili.
 
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, inadaiwa kuwa wapo walimu wakuu wa shule kadhaa wanaofikia hatua ya kuwatuhumu wanafunzi hao kwa makosa ya utovu wa nidhamu na kuwaeleza walezi na wazazi kuwahamisha ama warudie darasa wanafunzi hao.
 
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosainiwa na Kamishna wa Elimu, Dkt. Edicome Shirima, shule zote zilizofanya hivyo zimetakiwa kuwaruhusu wanafunzi hao kurejea shuleni Januari 20, mwaka huu ili waendelea na madarasa waliyopaswa.
 
Aidha wizara hiyo ya elimu imewakumbusha wamiliki na waendeshaji wa shule wote kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya elimu nchini.
 
SOMA TAARIFA RASMI HAPA CHINI.
1

2

Post a Comment

0 Comments