habari Mpya


Miongoni mwa Habari zilizosikika Saa Sita Mchana Radio Kwizera FM.

Source: RK, Ak (damu)
Ed: AG
Date: Monday, January 15, 2018
BUKOBA

Wakazi mkoani Kagera wametakiwa kujenga tabia ya kujitokeza kuchangia damu katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma ya damu mko ili kuokoa maisha ya wananchi wanaopoteza maisha kutokana na kupungukiwa damu

Hayo yameelezwa na makamu mwenyekiti wa umoja wa wanawake waombaji kanda ya ziwa Bi.Christina Mwainunu wakati akizungumza na redio kwizera baada kikundi chake kujitokeza katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kagera kutoa damu

Amesema kuwa kilichowasukuma kutoa damu ni kutokana na kusikitishwa na taarifa za wanawake, watoto na watu wengine wanaopoteza maisha kwa kukosa damu 

Insert……..Christina Mwainunu
Cue in…….
Cue out…...

Kwa upande wake kiongozi wa timu ya kukusanya damu mkoani Kagera Bw.Amos Mashweka amewapongeza wanawake hao kwa kuona umuhimu wa kuchangia damu ili kunusuru maisha ya wagonjwa na kuitaka jamii kuendelea kujitokeza kuchangia damu

Source: RK, JOVIN (ajari yaua watu 11)
Ed: AG
Date: Monday, January 15, 2018

BIHARAMULO

Watu wawili wamefariki wakati wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali teule ya wilaya ya Biharamulo na kufikisha idadi ya watu 11 kufuatia ajali ya gari iliyotokea jana katika kijiji cha Mugera kata ya Nyantakara wilayani Biharamulo mkoani Kagera

Mganga mkuu wa hospitali teule ya wilaya ya Biharamulo Dr. Gresimus Sebuyoya amesema kuwa majeruhi waliofikishwa hospitalini walikuwa saba lakini wawili walifariki muda mfupi kutokana na kuvuja damu nyingi

Aidha amesema kuwa watu tisa walifariki papo hapo mara baada ya ajali kutokea majira ya saa kumi za jioni na majeruhi watano waliobakia wanaendelea kupatiwa matibabu

Insert….Dr Sebuyoya
Cue in…..
Cue out…..

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Augustino Olomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyohusisha Haice yenye namba za usajiri T542 DKE iliyogongana na magari makubwa matatu yenye namba za usajiri T 147 DUJ, T 860 CGS na T 103 CGS


Source: RK, em (Uhaba wa matundu ya vyoo)
Ed: AG
Date: Monday, January 15, 2018

KARAGWE

Mwalimu mkuu wa Shule ya msingi Runyaka iliyoko wilayani Karagwe Mkoani Kagera Bw Desdery Costantine amesema shule inahitaji matundu mapya 30 ya vyoo ili kufunga matundu 20 yaliyopo kwa sasa kwani yanakalibia kujaa

Bw Costantine amesema kuwa shule hiyo yenye wanafunzi 722 huenda ikakumbwa na magonjwa ya mlipuko ikiwa hatua za dharura hazitachukuliwa kwani hata mwitikio wa wananchi kuchangia miundombinu ya shule ni mdogo kutokana na sera ya elimu bila malipo

Insert………………Bw Costantine
Cue in……………….Kwa sasa
Cue Out………….vyoo

Nao baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wamesema kuwa kutokana na vyoo hivyo kujaa wanasumbuliwa na harufu chafu inayokuwa ikitoka kwenye vyoo hivyo kwani hata wakifanya usafi hakuna unafuu wanaoupata

Hivi Karibuni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe Bw Wallence Mashanda akizungumza na wandishi wa habari, aliwataka wananchi kusaidiana na Serikali kuboresha miundo mbinu ya shule ili wanafunzi waweze kuyafurahia masomo yao


Source: RK, LT (Wizi)
Ed: AG
Date: Monday, January 15, 2018

KINSHASA

Kiongozi wa soko kuu katika mji wa Baraka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amewataka vijana kuachana na tabia ya kuiba mbao ambazo zimejenga vibanda pamoja na meza za biashara kwani ni kurudisha nyuma maendeleo ya soko hilo

Bw. Alenga Muhochu amesema wapo vijana wanaoiba mbao na miti ndani ya soko kwa lengo la kuwasha moto nyakati za usiku kwenye misiba hivyo ameiomba serikali kuingilia kati swala hilo

Insert…..ALENGA
Cue In: ndio wanakuja kuvunja soko…
Cue Out…sikitiko langu ni hilo.

Kwa upande wake mkuu wa sekta ya Mutambala Bw. Luhanusha Josué amekemea vikali hatua hiyo ya vijana kujihusisha na vitendo vya wizi na kwamba serikali itawachukulia hatua kali wale watakaokamatwa wakiiba 

Aidha Bw. Luhanusha amesema soko ni moja kati ya vitega uchumi vya serikali na linasaidia kwa kiwango kikubwa maendeleo ya mji, hivyo ameagiza uongozi wa jeshi la polisi tarafa ya Fizi kupanga askari watakao husika na ulinzi nyakati za usiku kwenye soko hilo

Post a Comment

0 Comments