habari


Miongoni mwa Habari zilizosikika Saa 24 zilizopita Radio Kwizera FM.

Source: RK, EE (pamba)
Ed: FM
Date: Friday, January 26, 2018

 SENGEREMA

Takribani hekari sita za zao la pamba zimeharibiwa na mvua ya mawe inayoendelea kunyesha katika kijiji cha Kishinda kata ya Tunyenye Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza

Wakiogea na radio kwizera baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamesema mvua zinazoendelea kunyesha wilayani Sengerema ndio chanzo cha zao hilo kuharibika kutokana mvua hiyo kuambatana na mawe pamoja na upepo

Aidha kufuatia zao hilo kuharibiwa wananchi hao wameiomba serikali kuwaangalia upya ikiwemo kuwaseheme kulipa mbegu walizokopeshwa

Insert…..wananchi
Cue in…..
Cue out….

Naye afisa mtendaji wa kijiji cha Kishinda Bw Samson Peleka amesema kuwa amewashauri wananchi kusubiri ushauri wa wataalam kutoka idara ya kilimo kuamua nini kifanyike kwa mazao hayo kwakuwa mvua bado zinaendelea

Source: RK, EM (Kurejesha mikopo)
Ed: FM
Date: Friday, January 26, 2018
 
KARAGWE

Imeelezwa kuwa ili vikundi vya akina mama vijana na walemavu Wilayani Karagwe Mkoani Kagera viweze kuendelea kunufaika na mikopo inayotolewa na halmashauri ya wilaya hiyo kupita asilimia tano za mapato ya ndani, vikundi hivyo vimetakiwa kurejesha mikopo hiyo kwa wakati 

Haya yamebainishwa na mkuu wa Wilaya ya Karagwe Bw Godfrey Mheluka Mara baada ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 60 na laki nane kwa vikundi 3o vya akina mama walemavu na vijana 

Bw Mheluka amesema asilimia tano za mapato ya ndani zinazotolewa na halmashauri  kila mwaka zinalenga kuwakomboa wananchi wa hali ya chini na pale kikundi kinaposhindwa kurejesha kwa wakati kinasababisha  vikundi vingine kushindwa kupata mikopo

Insert………………..Mheluka
Cue in……………….Wale wote
Cue Out………………hii

Awali Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii Wilayani Karagwe Bi Adeodata Peter akisoma taarifa ya maendeleo ya shughuli za idara hiyo amesema idara inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na baadhi ya vikundi kutorejesha mikopo kwa mujibu wa mkataba hasa vikundi vya vijana pamoja na mtaji mdogo usiotosheleza mahitaji ya waombaji

Source: RK, GM (afya)
Ed: FM
Date: Friday, January 26, 2018

BUKOMBE

Mila potofu, elimu na umbali wa vituo vya afya Wilayani Bukombe Mkoa wa Geita zimetajwa kuwa miongoni mwa sababu za baadhi ya akimamama wajawazito kushindwa kujifungulia katika vituo vya afya pale wanapopatwa na uchungu.

Hayo yamebainishwa na Mganga Mfawidhi wa Kituo cha afya cha Uyovu Dr Steven Kazuzu wakati akizungumza na waandishi wa habari wilayani humo   ambapo amesema uelewa wa wananchi kuhusu kujifungulia kwenye vituo vya afya ni mdogo hali inayopelekea wengi wao kujifungulia nyumbani

Hata hivyo Dr Kazuzu ameongeza kuwa Wanawake wengine wamekuwa na imani potofu na kwamba Mwanamke anapojifungulia nyumbani kuna baadhi ya viungo hubaki navyo tofauti na akijifungulia hospitalini

Insert…………….Kazuzu
Cue……
Cue out……

 Nao Baadhi ya wanawake wamesema tatizo kubwa ni ukosefu wa elimu na vifaa kwenye baadhi ya zahanati hali inayosababisha wengi wao kutoona umuhimu wa kujifungulia kwenye vituo vya afya

Source: RK, FB (Maandalizi mwenge)
Ed: AG
Date: Friday, January 26, 2018

NGARA

Watendaji wa vijiji na kata wilayani Ngara mkoani Kagera wametakiwa kuhamasisha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya ujio wa mbio za mwenge wa uhuru zinazotarajiwa kuanza mwezi wa Aprili mwaka huu


Agizo hilo limetolewa na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ngara Bw Aidan Bahama katika mkutano wa kikao cha pili cha maandalizi ya kuupokea mwenge wilayani humo ambapo amesema hesabu za makusanyo ya fedha ziwasilishwe kila Ijumaa

Insert…mkurugenzi
Cue in….kwahiyo watendaji wangu
Cue out…..wanangara wote

Naye mkuu wa wilaya ya Ngara Luten Kanal Michael Mtenjele amesema mwenge wa uhuru kiwilaya utakimbizwa kuanzia kata ya Kasulo hadi Ngara mjini kutokana na kwamba hauruhusiwi kukimbizwa zaidi ya kilometa 100

Insert…mkuu wa wilaya
Cue in….mwenge tunatakiwa tuukimbize
Cue out....tuondoke muda ambao ni mzuri

Mwenge wa uhuru wilayani Ngara unatarajiwa kuzindua na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo uwekaji wa jiwe la msingi katika vyumba vinne vya madarasa, ufunguzi wa duka la dawa la wilaya pamoja na uzinduzi wa kituo cha Mabasi na Magari madogo Benaco

Source: RK, SD (Kilimo)
Ed: AG
Date: Friday, January 26, 2018

KAHAMA

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Terack amewataka maafisa ugani katika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama kuhakikisha wanatembelea wakulima na kuwaelekeza namna ya kupambana na wadudu wanaoshambulia mazao ya chakula na Biashara

Akizungumza kwenye ziara ya kutembelea mashamba ya wakulima katika kata ya Mwakata ndani ya halmashauri ya Msalala amesema kuwa ni wajibu wa kila afisa ugani kuwatembelea wakulima na kutoa ushauri wa namna ya kupambana na wadudu hao

Amesema kuwa mkoa wa Shinyanga wadudu wengi hushambulia Mahindi na Mtama na kwa baadhi ya wakulima ambao hawajapulizia dawa huenda wakapata hasara

Kwa upande wake afisa kilimo katika halmashauri ya Msalala Bw. Zedekia Solomon amesema kuwa halmashauri hiyo ilipanga kulima hekta elfu 45 lakini hadi sasa wakulima wamelima hekta elfu 30 na mashamba yote yako vizuri


Source: RK, LT (Mateka)
Ed: AG
Date: Friday, January 26, 2018

KINSHASA

Jumla ya wanamgambo 15 wanaomtii Jenerali muasi amri William Yakutumba wamejisalimisha kwa jeshi la taifa na silaha sita zimekamatwa wakati wa oparesheni inayoendelea ya kuwasaka wanamgambo wa Maimai katika tarafa ya Fizi mashariki mwa DRC

Hayo yameelezwa na msemaji wa oparesheni Sokola ya pili Kapeteni Die-Donne Kasereka na kuwataka wanamgambo hao kuweka silaha chini na kujisalimisha ili kujenga nchi yenye amani na usalama

Kapteni Kasereka amesema tangu oparesheni ianze mwanzoni mwa wiki hii tayari jeshi la taifa limeshavikomboa vijiji vingi ambavyo vilikua vimeshikiliwa na wanamgambo wa Maimai vikiwemo vya Kazimia, Kikonde, Nemba, Mizimu, Talama na Yungu

Insert: Kasereka
Cue In: ndiyo batu yetu bako Kazimia, tunaendelea kusonga mbele…
Cue Out.…wakaaji waendelee kutuunga mkono.

Kwa upande wake Bw. Kashindi Majaliwa ambaye ni kiongozi wa shirika la raia katika mji wa Kazimia amelipongeza jeshi la DRC kwa kudhibiti mji huo, na kuomba liendelee kuwalinda raia na mali zao


Post a Comment