habari Mpya


Mbunge Gashaza aongoza Uzinduzi wa Kampeni za CCM Uchaguzi mdogo Udiwani Kata ya Keza-Ngara/Kagera.

26168233_1584522711636489_2433520063833496603_n
Mbunge wa Jimbo la Ngara,mkoani Kagera Mhe.Alex Gashaza mwenye shati la njano akiserebuka vilivyo  burudani wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za CCM Jana January 2,2018 kwenye Uchaguzi mdogo wa Madiwani katika Kata ya Keza utakaofanyika January 13,2018. Wengineo ni Wanachama wa chama hicho cha Mapinduzi.

26165841_1584522588303168_788135392786706233_n

26230320_1584520121636748_6146524611052549995_n
Bw.Issa Samma kushoto akifatilia mambo mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za CCM kwenye Uchaguzi mdogo wa Madiwani katika Kata ya Keza wilayani Ngara utakaofanyika January 13,2018. Wengineo ni Wanachama wa chama hicho cha Mapinduz.

26229401_1584444921644268_6271872905214614273_n
Mbunge wa Jimbo la Ngara,mkoani Kagera Mhe.Alex Gashaza toka kushoto,Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ngara ,George Rubagora na Wanachama wengineo wakifatilia mambo wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za CCM kwenye Uchaguzi mdogo wa Madiwani katika Kata ya Keza wilayani Ngara utakaofanyika January 13,2018.

26166659_1584445131644247_817661497912222053_n

26112453_1584522481636512_1608424464696505364_n
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa uchaguzi mdogo wa madiwani katika Kata hiyo Keza wilayani Ngara,mkoani Kagera kuwa utafanyika January 13,2018. 
 
Tume ilitangaza uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43  kuwa unafanyika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya madiwani kufariki dunia, kujiuzulu, kutohudhuria vikao na wengine ushindi wao kutenguliwa na Mahakama.
 
Tume imetangaza kufanyika kwa uchaguzi huo mdogo, baada ya waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa kuitaarifu tume uwepo wa nafasi wazi za madiwani katika kata hizo 43 zilizoko katika halmashauri mbalimbali 36 na mikoa 19 ya Tanzania Bara.
 
Kifungu cha 13 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya. 292 kinampa mamlaka waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kuitarifu tume kuhusu kuwepo kwa uchaguzi huo mdogo wa madiwani. 
 
Kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa; Sura ya 292, Tume ya taifa ya uchaguzi ina wajibu wa kuitisha na kuendesha Uchaguzi mdogo katika Kata hizo.
 
Aidha  Vyama vya Siasa, Wadau wote wa Uchaguzi na Wananchi wanakaribishwa kwa ajili ya kushiriki kwenye uchaguzi huo utakaozingatia ratiba iliyoainishwa.
 
Mwito kwa vyama vya Siasa na Wadau wote wa Uchaguzi kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Madiwani) za mwaka 2015, Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 pamoja na maelekezo yote yaliyotolewa au yatakayotolewa na Tume wakati wote wa Uchaguzi mdogo.

Post a Comment

0 Comments