habari Mpya


Mbaroni kwa Kujiunganishia Bomba la Mafuta ya Dizeli nyumbani kwake Mali ya TPA.


Askari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), wakishirikiana na Jeshi la Polisi nchini, wanamshikilia Ndugu Samwel Nzagi Kilang'ani mwenye umri wa miaka (63), kwa tuhuma za kutoboa bomba la mafuta ya Dizeli la "Single Point Mooring" mali ya TPA na kujiunganishia bomba lake la mafuta hadi nyumbani kwake ambako ameweka mantaki makubwa ambayo ameyachimbia chini ya ardhi.


Msemaji wa TPA,  Janeth Ruzangi amethibitisha kukamatwa kwa mtu huyo huku polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ikiendelea kumshikilia kwa uchunguzi zaidi.


Post a Comment

0 Comments