habari Mpya


Mapinduzi CUP 2017/2018-Simba SC yaambulia Sare dhidi ya Mwenge.

IMG-20180102-WA0063-640x640
Simba SC imebanwa na kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 ikicheza mechi ya kwanza Mapinduzi Cup 2017/2018 dhidi ya Mwenge FC kwenye uwanja wa Amaan, mjini Zanzibar.
 Jamal Mwambeleko alianza kuifungia Simba SC bao dakika ya pili (2) akiunganisha kwa kichwa krosi ya Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ lakini Mwenge walisawazisha dakika ya 28 goli likifungwa na Homoud Abrahman.
 
Kikosi cha Simba SC kilichocheza dhidi ya Mwenge kilisheheni wachezaji wengi ambao hawapati nafasi kwenye kikosi cha kwanza. Emanuel Mseja, Zimbwe Jr, Mlipili, Mwambeleko, Moses Kitandu, Said Ndemla.
singida%2Bunited
Mapema kabisa - Timu ya Singida United, ilifanikiwa kuianza vizuri michuano hiyo  ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuitandika Zimamoto FC kwa  ushindi wa mabao 3-2.
 
Mabao ya Singida United ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza michuano huyo yamefungwa na Deus Kaseke katika dakika ya saba, Dany Usengimana dakika ya 21 pamoja na Kigi Makasi dakika ya 81.
 
Kwa upande wa Zimamoto  mabao yake yote mawili yamefungwa na Ibrahim Elika katika daika ya 39 na 84.
 
Usiku huu Kikosi cha Young Africans kiko dimbani kucheza dhidi ya Mlandege wanaoongoza kundi hilo kwa Pointi 6.

Post a Comment

0 Comments