habari Mpya


Madarasa na Ofisi Vilivyoezuliwa na Upepo mwaka 2013 Shule ya Msingi Rwimbogo Kulikoni.??

1
Madarasa  Yalivyoezuliwa na upepo mwaka 2013.
 
 Walimu wa shule ya msingi Rwimbogo kata ya Muganza wilaya ya Ngara mkoani Kagera wameiomba Serikali ya kijiji cha Mukalinzi na Halmashauri ya wilaya ya Ngara kukarabati vyumba viwili vya madarasa  na ofisi yao   vilivyoezuliwa na upepo mwaka 2013.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo  Judah Sayi akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea shule hiyo January 26,2018  alisema shughuli za ufundishaji na ujifunzaji kwa walimu saba  na wanafunzi 552 zinakabiliwa na uhaba wa madarasa.
 
Sayi alisema shule hiyo kwa sasa inahitaji kuwa na madarasa 13 yaliyopo ni saba kwa uwiano wa chumba kimoja  wanafunzi 45 nakuhitaji madarasa sita ya ziada ambapo chumba kimoja kinakaliwa   wanafunzi 80 na msongamano ni  mkubwa.
2
3
Madarasa haya yalijengwa mwaka 1953 yalikuwa imara kuta zake lakini kutokana na kujengwa mlimani uliibuka  upepo na kuezua paa na kusababisha wanafunzi na walimu kukimbilia majengo mengine” Alisema Sayi.
 
Amesema tangu kuezuliwa kwa vyumba viwili na ofisi ya walimu umekuwa na  usumbufu wa walimu kusongamana kwenye  chumba cha maktaba na veranda na kusahihisha madaftari ya wanafunzihali ambayo inakatisha tamaa kazi ya ualimu.
4
5
Mahitaji  mengine  ni uhaba wa matundu ya vyoo, yanahitajika 13 upungufu matundu sita na nyumba nane kati ya 12 zinazohitajika ambapo alishauri serikali ya kijiji na halmashauri kuboresha miundombinu ya shule hiyo.
 
Katika hatua nyingine  wanafunzi wa shule hiyo wameiomba serikali kuwapatia mwalimu wa kike  wakuweza kusikiliza changamoto zao za kimaumbile kwani wanakuwa na aibu kuzieleza wazi mbele ya walimu wa kiume.
 
Wanafunzi na walimu wa kiume walisema aliwahi kuletwa mwalimu wa kike  shule ya msingi Rwimbogo lakini kutokana na kuwepo matukio ya ujambazi na watu kuuawa na wengine kujeruhiwa mwalimu huyo alihamia sehemu nyingine.
 
Mmoja wa walimu wa Shule hiyo Andrea Gabriel aliyekuwa akisahihisha  madaftari ya wanafunzi kwenye veranda ya chumba cha maktaba, aliomba serikali kujenga ofisi ya walimu kuepukana na usumbufu wa mvua kulowanisha madaftari
6
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mukalinzi,Bw.Richard Magogolo amesema wananchi wameanza kuchangia Sh 2000 kila Kaya kukarabati vyumba hivyo ingawa michango inasuasua  kutokana na maagizo ya serikali ya kuifuta. 
 
Amesema mkakati mkubwa wa wananchi ulikuwa ni kujenga kituo cha polisi kuimarisha ulinzi na usalama ambapo kituo hicho kimefikia hatua ya renta kwa thamani ya Sh8 milioni na malengo  hadi kukamilika kitagharimu Sh15 milioni  
 
Akizungumza katika kikao cha Walimu Wakuu, Maafisa Elimu Kata na Watendaji wa Kata hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara, Bw. Aidan Bahama amesema iwapo wananchi wataanzisha miradi kwa kuweka vifaa vinavyopatikana kwenye mazingira yao  serikali itapeleka fedha kuwaunga mkono
7

Post a Comment

0 Comments