![]() |
Vikombe vya Ubingwa.
|
![]() |
Mwenyekiti wa Kumuyange FC ya Ngara,Ezron Nyamunda akishangilia Ubingwa na Kombe lao.
Timu ya Kumuyange
FC ya Ngara imeibuka Bingwa wa Soka mkoani Kagera 2017 /2018 baada ya kumvua
Ubingwa huo Timu ya Eleven Stars ya Misenyi kwa kumfunga magoli 5-1,mechi ikichezwa uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Ushindi huo
unawafanya Kumuyange FC kuandika rekodi ya kuubeba Ubingwa wa Mkoa bila
kupoteza mechi yake hata moja,ikishinda zote toka hatua ya makundi na ligi
ndogo na sasa inaubeba Ubingwa kwa kujikusanyia Pointi 9.
Kumuyange FC
walipata ushindi kwa Goli za Ezekiel Aizaki dk 3, Dennis Msuva la dk 44, 47, na
73 na la 5 likifungwa Ibrahim Kungu dk 81 wakati Eleven Stars likifungwa na Emanuel Sam dk 27.
|

![]() |
Furaha ya Ubingwa ikiendelea kwa Timu ya Kumuyange
FC ya Ngara.
|

![]() |
Mashabiki wa Eleven Stars wakiwa hawaamini kinachotokea kwa Timu yao dhidi ya Timu ya Kumuyange
FC ya Ngara baada ya kumvua
Ubingwa huo Timu ya Eleven Stars ya Misenyi kwa kumfunga magoli 5-1.
|
![]() |
Timu ya Kumuyange
FC ya Ngara.
|








![]() |
Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Ngara -NDFA sambamba na Mwenyekiti wa Timu ya Kumuyange
FC ya Ngara wakifurahia Ubingwa wa Soka mkoani Kagera 2017 /2018 baada ya kumvua
Ubingwa huo Timu ya Eleven Stars ya Misenyi kwa kumfunga magoli 5-1 Jana January 14,Kaitaba Bukoba.
|
![]() |
Said
Mazagazaga mwenye shati la kijani akipokea Kombe na Zawadi ya Seti moja
ya Jezi na Mpira mmoja baada ya kuibuka washindi wa Pili.
Mchezo wa
mchana saa nane, Mazagazaga FC ya Biharamulo imeshika nafasi ya pili kwa
kujiongezea point na kufikisha 4 baada ya kuifunga Vatican FC ya Muleba mabao
2-1.
Goli mbili
za Huruma Shamba dk ya 2 na 34 akiipa Mazagazaga FC ushindi huo huku lile la
Vatican FC likiwekwa kambani na Nelson Richard dk ya 53 kipindi cha pili kwa
njia ya penati.
Eleven Stars
imemaliza kwa kushika nafasi ya 3 na Pointi 4 huku ikifungwa mabao mengi
tofauti na Mazagazaga FC na Vatican FC ya Muleba ikiburuza bila Pointi baada ya
kufungwa mechi zote 3.
Kumuyange FC
ilikabidhiwa Kombe la Ubingwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi-CCM Manispaa
ya Bukoba, Bw. Muganyizi Zachwa sambamba na Jezi seti moja na Mipira miwili.
|

0 Comments