habari Mpya


Korea yafanya Majaribio ya Usalama Kujiandaa na Olimpiki.

Mazoezi ya kudhiti usalama yalipokuwa yakifanyika.

Korea Kusini imefanya majaribio kadhaa ya ulinzi na usalama katika eneo la Pyeongchang ambako kutafanyika michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi kwa siku 16 kuanzia Februari 9 hadi 25 mwaka huu.

 Waandaaji wa michezo hiyo wamesema sababu kubwa ya majaribio hayo ni hofu mpya ya ulinzi kwenye mji huo, kutokana na ushiriki wa ndugu zao Korea Kaskazini.
Majaribio hayo yamefanyika katika hafla maalum ya uzinduzi wa vikosi vya ulinzi na usalama vitakavyotumika wakati wa Olimpiki hiyo.

Korea Kaskazini inapeleka timu kubwa kwenye mashindano hayo kama sehemu ya upatanishi wa kidemokrasia uliofikiwa hivi karibuni hali ambayo inawalazimu Korea Kusini kuimarisha zaidi ulinzi kwenye maeneo yao.

Mbali na wanariadha, Korea Kaskazini itapeleka pia maafisa, vikundi vya ushangiliaji na sanaa za maonesho mengine pamoja na watoa burudani wa mchezo wa Taekwondo.

Rais wa kamati ya maandalizi ya mashindano hayo, Lee Hee-Boem amesema Korea Kaskazini itatuma msafara mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya Olimpiki hiyo hivyo ni vema wakajipanga vizuri katika suala la usalama.

“Wanaleta wanariadha 24, maafisa 24, pamoja na watu wengine. Hii itasaidia sana kuchangia kufika kwa ujumbe wa amani Pyeongchang lakini naamini kutakuwa na ongezeko la mambo mengi sana ya maandalizi yanayohusiana na usalama,” amesema Lee.

Post a Comment

0 Comments