habari Mpya


Zaidi ya Tani mbili za Samaki Zakamatwa na Jeshi la polisi wilayani Ngara mkoani Kagera.

Zaidi ya Tani mbili na nusu za Samaki aina ya Sangara na Sato mali ya Bw Ayubu Sanga zimekamatwa na Jeshi la Polisi wilayani Ngara mkoani Kagera katika tarafa ya Murusagamba.

Afisa Uvuvi mkoa wa Kagera Bw. Efrazi Mkama amesema Samaki hao wenye thamani ya shilingi milioni 20, laki 8 na elfu 25, walikuwa wakisafirishwa ndani ya gari kutokea manispaa ya Bukoba na wilaya ya Muleba kuelekea nchini Burundi kinyume cha taratibu.
Katika tukio hilo mkuu wa wilaya ya Ngara, Luteni Kanali Michael Mtenjele amekemea kitendo hicho huku akiwataka wananchi kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake na kutoa taarifa wanapo baini vitendo kama hivyo vya kimagendo.

Samaki hao waligawiwa kwenye taasisi mbalimbali ikiwemo Vituo vya polisi, vituo vya jeshi, shule ya sekondari Murusagamba pamoja na wananchi waliofika eneo la tukio.


Mpaka sasa Bw Ayub Sanga Pichani anashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Ngara mkoani Kagera kwa mahojiano zaidi na uchunguzi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.

Post a Comment

0 Comments