habari Mpya


Vijiji 21 wilayani Ngara kunufaika na Umeme wa REA Awamu ya Tatu.

26165881_1771589669581086_384101279604620159_n
Waziri wa Nishati wa Tanzania ,Medard Kalemani (akiwa eneo la mitambo ya kufua umeme Nakatunga, Ngara ) ametoa agizo kwa mkandarasi anayejenga mradi wa Umeme wa grid ya Taifa katika wilaya za Ngara na Biharamulo kukamulisha mradi huo ifikapo Mwishoni mwa Mwezi Januari 2018.

Waziri Kalemani ametoa agizo hilo hii leo wakati wa ziara yake katika wilaya hizo baada ya kupatiwa taarifa za ujenzi wa mradi huo kutoka kwa kaimu meneja wa Tanesco wilayani Ngara, Mhandisi Felix Olangi ambaye amedai tangu kuanza kwa ujenzi miezi mitano iliyopita umefikia 69%.
 
Waziri Kalemani amesema vijiji vyote nchini havitarukwa kupata umeme na kuhakikisha serikali inapungua gharama za kuzalisha umeme wa mafuta ambapo imeelezwa wilaya ya Ngara hutumia Sh 240 milioni kwa mwezi.
 
Amesema shirika la Tanesco Wilaya na Mkoa wasimamie mkandarasi huyo aharakishe kukamilisha mradi wa umeme na wananchi wanufaike kwa kuanzisha miradi ya kiuchumi kwa kutekeleza kauli ya serikali ya Tanzania ya viwanda.

25994677_1771589979581055_4809816261258659775_n

26165176_1771589569581096_4529735281864420324_n
Awali Kaimu Meneja wa Tanesco wilayani Ngara, Felix Olang amesema mradi wa umeme wa gridi ya Taifa utanufaisha vijiji vinane vya wilaya hiyo na viwili katika wilaya ya Biharamuloambao utakuwa wa kilovoti 33 katika umbali wa kilomita 69.5.
 
Aidha amesema umeme wa REA awamu ya tatu utanufaisha vijiji 21 wilayani Ngara na wataunganishiwa wateja 1733 wlioko kwenye mkondo wa kilomita 63.3 na kwa wilaya ya Biharamulo ni vijiji 32 vyenye wateja 2729 walioko katika kikomita 84.82.
26167547_1771590119581041_53418876507390261_n
Katika hatua nyingine Mbunge wa jimbo la Ngara Alex Gashaza amemuomba Waziri kalemani kusogeza huduma ya umeme katika kata ya Bukiriro Bugarama na Murusagamba palipo na vituo vya Afya na Zahanati na taasisi nyingine za Serikali.
 
Amesema katika kituo cha Afya Murusagamba na Bukiriro kunatarajiwa kutolewa huduma za upasuaji katika sekta ya afya kwa wagonjwa wakiwemo wajawazito na kwamba serikali imetoa Sh700 milioni kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya vituo hivyo.
 
Amesema katika kata hizo pia zipo shule ya sekondari za Bukiriro, Kibogora, Muganza na Murusagamba yenye wanafunzi wa bweni wa kidato cha tano na kwamba umeme wa kwenda Murusagamba unaweza kuchotwa Nyakahura wilayani Biharamulo umbali wa kilomita 14.
26166431_1771589756247744_1856055154086868938_n
Waziri Kalemani akiwa ziarani wilayani Ngara Mkoani Kagera ametembelea kijiji Nterungwe ambacho kitapatiwa mradi wa umeme wa REA awamu ya tatu pamoja na kijiji cha Rwakalemela, Benako kutakapojengwa kituo ch kupozea umeme wa Gridi ya Taifa pamoja na vijiji vya Nyabugombe na Kikomakoma wilayani Biharamulo Mkoani humo.

Post a Comment

0 Comments