habari Mpya


Taswira Picha Ajali K9-Ngara ,Dereva na Tingo wake wakitoka salama bila kuamini.

Ajali hii imetokea Usiku wa Kuamkia Jumapili December 17, 2017 eneo la mteremko wa K9 Kijiji cha Kasharazi wilayani Ngara mkoani Kagera ambapo ajali mbili zilitokea kwa wakati tofauti zikisababishwa moja ni kufeli kwa mfumo wa breki hasa hili lori pichani ambalo lilikuwa limebebe tani za mahindi.

Ajali ya pili ilisababishwa na kufeli kwa mfumo wa upepo ambapo Madereva wote wa magari hayo pamoja na matingo wao walipata majeraha madogo ya  mchubuko tu wa kawaida na hakuna kifo chochote.Kikosi cha Usalama Barabarani wilayani Ngara kinatoa wito kwa Madereva wote wanaotumia barabara kuu ya Benaco-Ngara-Burundi kuendelea kutii alama na sheria za usalama barabarani kuepuka ajali zinazoweza kuzuilika pamoja na kuokoa maisha yao na mali.


Post a Comment

0 Comments