habari Mpya


Mohammed Dewji Mwekezaji Klabu ya Simba SC.

24474554_1682958941744009_1070489159_o
Bilionea Mohammed Dewji, amepita katika mchakato wa uwekezaji wa klabu ya Simba SC na ofa yake ya Sh bilioni 20.

Dewji amejitokeza na kuwa muwekezaji pekee ambaye aliweka dau la Sh bilioni 20 kupata hisa asilimia 51.
Hata hivyo, baada ya mchakato huo makubaliano yalikuwa ni hisa 49 anazoruhusiwa kuchukua kwa kitita hicho cha Sh bilioni 20.
Mwenyekiti wa kamati ya mchakato huo wa mabadiliko, Jaji Mihayo amesema, Mo Dewji amepita na kitachofuatia ni majadiliano mengine baada ya mkutano wa leo December 3, 2017.
Mohammed Dewji ndiye mshindi, maana katika kamati yetu. Hivyo yeye ndiye amekuwa mshindi wa kuwania kuwekeza katika klabu ya Simba SC. Baada ya mkutano huu kutakuwa na majadiliano,” alisema.
Mkutano huo wa wanachama bado unaendelea Posta jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments