habari Mpya


Benaco FC Yaondoshwa Robo Fainali Ligi Daraja la 3 Mkoani Kagera.

26178899_1711063475600222_196576421_o
Wachezaji wa Mazagazaga FC wakishangilia kufuzu hatua ya nusu fainali na mashabiki wao kwenye uwanja wa Kemikimba,Benaco.
Timu ya Benaco FC imeshindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani kuvuka kihunzi cha robo fainali ya Ligi daraja la 3 mkoa wa Kagera 2017/2018 baada ya kukubali kuondoshwa kwa mbinde na Timu ya Mazagazaga kwenye mchezo wa hatua hiyo ili kupata timu mbili kutoa kituo cha Benaco zitakazokuja kucheza na timu mbili za kituo cha Muleba kupata Bingwa wa Soka wa Mkoa wa Kagera.

Mchezo huo uliopigwa Jana December 29,2017 katika uwanja wa Kemikimba mjini Benaco ukichezeshwa na mwamuzi wa kati Ligstone Lwiza akisaidiwa na Yahya Juma na Aneth Mathias umemaliza dakika 90 kwa mashabiki wa Benaco FC kushindwa kuamini kile Timu yao imekifanya kwa kushindwa kufungana bao hata moja na Mazagazaga FC.
26194642_1711063482266888_55015877_o
Benchi la Benaco FC licha ya mchezo kumalizika lilibaki bila kuamini kile kilichotokea.

26237668_1711063495600220_1035236487_o

26236137_1711063332266903_1987184378_o
Benaco FC sasa kaondoshwa kwa penati 4-1 na unakua msimu wake wa pili kushiriki ligi hiyo ambapo msimu wa 2016/2017 waliishia hatua ya makundi huku Golikipa wa Mazagazaga FC ,Charles Ubiksen akiokoa au kucheza penati 2 za Benaco FC.
 
Leo December 30, Jumamosi ni hatua ya robo fainali ya pili inachezwa kwa Kumuyange FC dhidi ya Mabingwa wa Mkoa wa 2015/2016 Murusagamba FC.

Post a Comment

0 Comments