habari Mpya


Wawili Wafariki Ajali ya Basi na Gari dogo , Singida.

2
Watu wawili wamefariki dunia baada ya gari aina ya Landcruise kuacha barabara na kuingia uvunguni mwa basi, lililokuwa upande kulia mwa barabara ya Singida-Dar es Salaam.

Ajali hiyo iliyotokea leo November 11, 2017 majira ya asubuhi,imelihusisha gari aina ya Landcruiser lenye namba za usajiri T 862 DJW lililokuwa likitokea Dar-es-salaam kuelekea Mwanza na basi  mali ya kampuni ya Taqwa Coach Ltd ya Dar-es-salaa lenye namba za usajiri T 159 CWH.
 
Ajali hiyo imetokea katika eneo la kijiji cha Kideka kata ya Puma wilaya ya Ikungi, mkoani Singida.

1

3
Kaimu Kamanda Jeshi la Polisi,mkoa wa Singida,Isaya Mbughi,amesema miili ya abiria hao wa Landcruiser ambao majina yao wala makazi yao bado hayajulikana,imehifadhiwa katika hospitali ya Misheni Puma.
 
Mbughi amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa kuna kila ya dalili dereva wa Landcruiser alikuwa amelala,na hivyo gari lilihama kutoka upande wa kushoto na kwenda kulia.
Kaimu kamanda huyo,amesema  Utingo wa basi hilo,amevunjika mkono,na mtoto mmoja mwenye umri kati ya miaka sita na saba,naye amejeruhiwa na wote wamelazwa katika hospitali ya Misheni ya Puma.

4

Post a Comment

0 Comments