habari Mpya


Wanangara wang'ara Mbio za Kilimanjaro International Airport Marathon 2017.

23659531_865309263628953_607101731744357670_n
Washiriki wa Ngara Pichani kushoto, Kwa Mara ya kwanza katika mbio za Kilimanjaro International Airport Marathon 2017 katika Picha ya Pamoja na Afisa Michezo Mkoa wa Arusha Bw.Benson Maneno -Kulia, –David Mabula Mapembe alishika nafasi ya 24 ,upande wa wanaume akitumia saa moja dakika 13 na sekunde 05 na Mwl Edward John akishika nafasi ya 30 kwenye mbio za kilometa 21, kati ya Washiriki 2000, wanaume akitumia saa moja dakika 36 na sekunde 00.

Mashindano  hayo ya mbio za Kilimanjaro International Airport Marathon, yamefanyika kwa mara ya kwanza wilayani Hai mkoani Kilimanjaro na kushuhudiwa wanariadha wa Kenya waking'ara katika mbio za kilomita 42 na 21.
23722499_1336051963172897_5777496100136868557_n
Katika mbio za kilomita 42, nafasi ya kwanza hadi ya tatu zimeshikwa na wanariadha kutoka Kenya ambapo  Duncan Kwemboi ameibuka kidedea kwa kutumia saa mbili dakika 19 na sekunde 10 kwa wanaume huku Gladys Otero akiongoza mbio hizo kwa wanawake akitumia saa 2 dakika 49 na sekunde 32.
 
Katika mbio za kilomita 21, Joel Kipmatai ameshinda kwa upande wa wanaume akitumia saa moja dakika 6 na sekunde 19 huku upande wa wanawake Merci Kibarus pia kutoka Kenya akiibuka kidedea kwa kutumia saa 1 dakika 15 na sekunde 40 huku nafasi ya tatu ikishikwa na mtazania Failuna Abdi ambaye amezidiwa sekunde  13 na mshindi wa kwanza.
 
Washindi katika mbio hizo wamejinyakulia zawadi za fedha taslimu shilingi milioni tano kwa mshindi wa kilomita 42 na milioni 3 kwa mshindi wa kilomita 21.

Post a Comment

0 Comments