habari Mpya


Wanafunzi Watano wa Shule ya Msingi Kihinga,Ngara wafariki kwa Bomu wakiwa Shuleni.


23423470_1656632827709954_505482464_o
Wanafunzi wa Tano  wa Shule ya msingi Kihinga,iliyopo wilayani Ngara  mkoani Kagera wamefariki dunia na wengine 42 wamejeruhiwa baada ya kulipukiwa na bomu la kutupwa kwa mkono  na wamelazwa Hospitali ya misheni Rulenge wilayani humo .

Mganga Mkuu wa hHospitali ya Rulenge, Sr Goleth Fredrick amesema idadi hiyo imeongezeka baada ya wengine kutolewa katika kituo cha afya bukiriro na kwamba wanafunzi wawili wamefariki wakati wakipatiwa Matibabu.
23432416_1656632857709951_1359203868_o
Madaktari wa Hospitali ya Mission Rulenge wakiendelea na Matibabu kwa Majeruhi.

Kamanga wa Jeshi la Polosi mkoani Kagera Agustino Olomi amesema chanzo cha wanafunzi hao kujeruhiwa kwa bomu ni zoezi la kuuza vyuma chakavu ambapo mwanafunzi aliliokota na kuja nalo shuleni ili alipeleke kwa mnunuzi na kupewa madaftari.

Hata hivyo Kamanda wa Kikosi cha Kulinda mipaka cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ wilaya ya Ngara ,Meja TR Mutaguzwa amesema Bomu hilo lilikuwa na vipande 36 na lingelipukia ndani ya darasa wangeleta athari zaidi .

Taarifa zaidi zinafuata
23468179_1656632777709959_1815028699_o

Post a Comment

0 Comments