habari Mpya


VPL 2017/2018 -Simba SC Yailaza 1-0 Tanzania Prisons.

1
John Bocco ameipa Simba SC ushindi wa kwanza dhidi ya Tanzania Prisons tangu iliposhinda mara ya mwisho 2013 kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya.

Bao pekee la ushindi limefungwa dakika ya 84 kipindi cha pili baada ya Bocco kuuwahi mpira uliochelewa kuokolewa na mabeki wa Tanzania Prisons.
Simba SC imepata pointi sita kwenye uwanja wa Sokoine baada ya kusubiri kwa muda mrefu.
Ushindi huo unaifanya Simba SC ifikishe pointi 22 ikiwa inaongoza ligi mbele ya Azam FC ambayo itacheza kesho dhidi ya Njombe Mji FC.
Yanga SC inabaki katika nafasi ya tatu huku Mtibwa Sugar ikiwa nafasi ya nne timu zote zikiwa na pointi 17 lakini zinatofautiana kwa wastani wa magoli. (Azam FC , Yanga SC na Mtibwa Sugar ni timu tatu ambazo zipo nafasi Nne za juu zikiifukuza Simba SC kileleni kwenye msimamo wa VPL 2017/2018).
Matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa leo Jumamosi Nov 18, 2017.
  • Stand United 0-0 Mwadui

  • Ruvu Shooting 1-0 Ndanda

  • Majimaji 2-1 Mbao

Post a Comment

0 Comments