habari Mpya


Vijana 57 wamehitimu Mafunzo Mgambo , Kata ya Bukiriro wilayani Ngara.

23634018_1663800463659857_1479426119_o
Vijana 57 wamehitimu mafunzo ya jeshi la akiba yaani Mgambo katika Kata ya Bukiriro wilayani  Ngara mkoani Kagera  hii Leo November 15,2017 kwa lengo la kuimarisha Ulinzi na Usalama.

Kati ya vijana hao 10 ni wa kike na mafunzo yalianza June 5 mwaka huu katani humo ambapo yamefungwa na Mkuu wa wilaya ya Ngara, Luteni kanali Michael Mntenjele .
23633460_1663800436993193_1524627755_o
Luteni Kanali Michael Mntenjele ( wa pili kutoka kulia pichani ) amewakata wahitimu hao wa Mgambo kuimarisha amani na utulivu kwa kudhibiti magendo maeneo ya mpakani na kushirikiana na vyombo vya dola kutokomeza uhalifu.

23633422_1663800440326526_503146687_o
Vijana hao wamesema katika mafunzo yao wamekumbana na changamoto za kutambua uzalendo, kujiandikisha wasiokuwa RAIA kutoka kata jirani ambao baada ya kuchujwa wamebaki watanzania watakaootumikia taifa kwa weledi mkubwa.

Post a Comment

0 Comments