habari Mpya


Taswira Picha Siku ya Wazi ya Radio Kwizera na Wadau.

Mgeni Rasmi katika Tamasha hilo la Wazi la Radio Kwizera-RADIO OPEN DAY  ,Katibu Tawala wilaya ya NGARA mkoani Kagera Bw. Vedastus Tibaijuka ( Pichani) pamoja na kuikubali Radio Kwizera  kama daraja la kuleta elimu ,habari na burudani kwa wananchi wa ngara hakusika kuwataka watumishi wake kufanya kazi kwa weledi ili kuzidisha kuwa daraja kati ya Serikali na Wananchi katika kuwafikishia Taarifa na Maendeleo yao.

Pichani Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri  ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera bw Aidan Bahama. 
 

Kutoka kulia ni Baba Askofu Severin Niwemugizi wa Jimbo Katoliki la Rulenge-Ngara sambamba na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara Bw.Aidan Bahama wakifatilia kinachoendelea  katika  siku  maalum ya kuwakutanisha wadau wa radio kwizera leo hii November 3, 2017 katika ukumbi wa Radio Kwizera.

Mkurugenzi wa Radio Kwizera Padre Damasi Missanga (Kushoto Pichani) katika  siku  maalum ya kuwakutanisha wadau wa radio kwizera leo hii November 3, 2017 katika ukumbi wa Radio kwizera amesema kuwa  amesema radio ni kiungo muhimu kati ya wananchi na serikali katika kutekeleza shughuli  mbalimbali hivyo viongozi wanaowajibu wa kuitumia radio kwizera kwani wakiitumia kuelimisha jambo litakuwa limewafikia wengi.

Mwl Robert Mkosamali pichani kulia  kutoka BBC MA pia alielezea ushirikiano baina ya BBC MA na Radio Kwizera katika kuandaa vipindi vyenye kugusa  Utawala bora ili kuleta uwajibikaji kwa Viongozi na jamii.


 Kulia ni Shehe wa Wilaya ya Ngara ,Rajab Msabaha akiwa Mwenyekiti wa CHADEMA -Ngara Kenedy Stanphord na Wadau wengine mbalimbali pichani chini kutoka  Serikali,Vyama vya Siasa,Viongozi wa Dini,Wafanya Biashara na Wananchi wakifatilia mambo wakati wa Siku hiyo ya Radio Kwizera ambapo walifanya Ziara ya kutembelea Vitengo mbalimbali vya RK na kupata maelezo yao.

Post a Comment

0 Comments