habari Mpya


Simba SC na Lipuli FC Ngoma yatoka Sare, VPL 2017/2018.

IMG_7721
Beki wa Simba, Mohamed Huesin (kushoto) akimtoka mchezaji wa Lipuli, Martin Kazila wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2017/2018 jioni ya leo November 26, 2017.

IMG_7722
Wekundu wa Msimbazi Simba SC wameshindwa kuutumia vizuri uwanjwa wa nyumbani wa uhuru, baada ya kulazimishwa matokeo ya sare ya kufungana bao 1-1 na Timu ya Lipuli FC ya Iringa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
 
Matokeo hayo ya  Sare , Yanamaanisha Simba SC inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 23 baada ya mechi 11, ikiwazidi kwa pointi mbili tu Mabingwa watetezi, Yanga SC walio na Pointi 21 nafasi ya 3 ambao nao jana November 25, 2017 walilazimishwa sare ya 1-1 na Tanzania Prisons Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
IMG_7782
 Wachezaji wa Simba SC wakishangilia.
 
Azam FC wako nafasi ya Pili na Pointi 22 na kama watashinda mechi yao ya Kesho Jumatatu November 27, 2017 dhidi ya Mtibwa Sugar walio nafasi ya  5 na Pointi 17 huenda wakarejea kileleni mwa Msimamo wa Ligi hiyo.
 

Katika mchezo huo uliochezeshwa Abdallah Kambuzi wa Shinyanga, aliyesaidiwa na Khalfan Sika wa Pwani na Vincent Mlabu wa Morogoro iliwachukua dakika 15 tu Simba SC kupata bao la kuongoza, lililofungwa na kiungo wake mkongwe, Mwinyi Kazimoto Mwitula.
 
Lipuli FC walifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika nne baadaye kupitia kwa Nahodha wao, Mghana Asante Kwasi aliyefunga kwa shuti la mpira wa adhabu.


IMG_7648
 Kikosi cha Lipuli FC.

IMG_7656
Kikosi cha Simba SC.

Post a Comment

0 Comments