habari Mpya


Majeruhi 33 kati ya 44 Waliojeruhiwa kwa Bomu,Ngara waruhusiwa Kutoka Hospitali.

23468114_1657880457585191_1102086839_o
Mganga mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera ,Dr Revocatus Ndyekobora amesema Majeruhi 33  kati ya 44 waliojeruhiwa kwa  bomu la kutupwa kwa mkono Novemba 8,2017 wameruhusiwa kutoka hospitalini baada ya afya zao kuimarika.

Aidha amesema Majeruhi  11 wamefanyiwa kipimo cha X Ray na Madaktari Bingwa kutoka Bugando/Mwanza na Hospitali ya Mkoa wa Kagera na kwamba wamewabaini kukutwa na vyuma ndani ya miili yao hivyo wataendelea kuchunguzwa zaidi kubaini kama vyuma vilivyomo  vinahitaji kutolewa ama la na kupatiwa matibabu zaidi.
23483163_1657880230918547_1367289644_o
Mkuu  wa wilaya  Ngara Luteni Kanali Michael Mtenjele.

 November 8,2017 Majira ya asubuhi ,Wanafunzi wa Tano  wa darasa la kwanza wa Shule ya msingi Kihinga,iliyopo wilayani Ngara  mkoani Kagera walifariki dunia na wengine 42 na mwalimu wao mmoja kujeruhiwa baada ya kulipukiwa na bomu la kutupwa kwa mkono  na kukimbizwa  katika Hospitali ya misheni Rulenge kwa matibabu zaidi.

 Msaada mkubwa unahitajika hasa wa - CHAKULA, MASHUKA/BLANKETI 50,MAFUTA KWA AJILI YA KUSAIDIA KUSAFIRISHA MAJERUHI WANAOHITAJI RUFAA KWENDA HOSPITALI NYINGINE PAMOJA NA DAMU SALAMA.

MSAADA WAKO WAWEZA UPELEKA MOJA KWA MOJA HOSPITALI YA MISSION RULENGE AU OFISI YA KATIBU TAWALA WILAYA YA NGARA.

TUENDELEZE KWA VITENDO UTAMADUNI WA UZALENDO WA KUSAIDIANA WAKATI WA MAAFA.
23468545_1657880394251864_1936723197_o

23469097_1657880227585214_57658431_o
Kufatia tukio hilo, Mkuu  wa wilaya  Ngara Luteni Kanali Michael Mtenjele (Aliyeweka mkono mfukoni) amepiga marufuku kuanzia sasa  kwa Wananchi kufanya biashara ya vyuma chakavu wilayani humo   na kila anayetaka kufanya shuguli  hiyo   ajisajili kwa kupata kibali  lakini sio kuhusisha wanafunzi wa shule za  msingi na sekondari.


Akiwa katika Hospitali ya Misheni ya Rulenge kuwajulia hali majeruhi alisema mbele ya wataalamu wa afya na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama kwamba  yeyote atakayetangaza biashara ya vyuma chakavu atashughulikiwa na vyombo vya dola.
23482881_1657880150918555_1081643267_o

Post a Comment

0 Comments