habari Mpya


Hali hii Mpaka Lini??Vyoo Vya Walimu wa Shule ya Msingi Kanazi –Ngara/Kagera.

24251003_1678731312166772_143545840_o
Hali ya Vyoo Vya Walimu wa Shule ya Msingi Kanazi  iliyopo wilayani Ngara mkoani Kagera ni mbaya na wanahofia kupatwa magojwa ya mlipuko wakienda haja huchunguliwa na wapita njia.
24210049_1678731475500089_1929915816_o

24201342_1678731568833413_2134959913_o
Walimu wa shule ya msingi Kanazi iliyoko wilaya ya Ngara mkoani Kagera wanakabiliwa na ukosefu wa vyoo katika mazingira ya shule hiyo pamoja na kwenye nyumba zao za kuishi na kusababisha wakumbwe na hofu ya kupata magonjwa ya mlipuko.
 
Wakizungumza na Radio Kwizera katika shule hiyo jana walimu hao wamesema wanadhalilika kwa kutumia choo ya mabanzi na kujengwa kwa miti kisha kukandikwa kwa udongo ambapo kimebomoka na kusababisha walazimike kukimbia kwenye nyumba za majirani ambazo pia hazina vyoo bora kiafya.

24271308_1678731232166780_93912078_o

24259539_1678731322166771_1278356938_o

24201342_1678731568833413_2134959913_o
Aidha Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Godefrey Rutakyamilwa wamesema uongozi wa shule kwa kutumia fedha za Ruzuku umetenga shilingi laki 2 na elfu 50 kwa ajili ya kununua matofali lakini walimu 15 wa shule hiyo wanahangaika kupata choo Insert Walimu.
 
Hata hivyo Afisa mtendaji wa kata ya Kanazi wilayani Ngara Bw Sprian Biherere amesema mkakati uliopo ni kujenga choo cha walimu kuanzia Januari 2018 na kwamba shule ni mali ya jamii inayotakiwa kuchangia vifaa vya ujenzi kutoka mazingira yanayowazunguka. 
 
Pamoja na hayo ameishauri idara ya elimu ya msingi katika wilaya ya ngara kutenga fedha za ruzuku kwa ajili ya kujenga vyoo imara na vilivyo bora kwa walimu na wanafunzi wa shule ya msingi kanazi
24201285_1678731142166789_1853789024_o

24201441_1678731238833446_2051894532_o

Post a Comment

0 Comments