habari Mpya


Elias Maguri aipa Taifa Stars Sare na Wenyeji Benin.

1
Timu ya Taifa ya Tanzania ,Taifa Stars imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji Benin katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa l'Amitie, au Urafiki mjini Cotonou leo November 12, 2017.

Katika mchezo huo, hadi mapumziko wenyeji The Squirrels, walikuwa mbele kwa bao 1-0.

Bao hilo lilifungwa kwa penalti na mkongwe mwenye umri wa miaka 33, Nahodha, Stephane Sessegnon anayechezea klabu ya Montpellier ya Ufaransa.
 
Sessegnon akamtungua kipa namba moja wa Tanzania, Aishi Manula kufunga bao lake la 21 timu ya taifa katika mechi ya 68.
 
Tanzania ilisawazisha kupitia  mshambuliaji wa zamani wa Simba SC ya Tanzania na Dhofar SC ya Oman, Elias Maguri aliyefunga bao hilo akimalizia krosi ya winga Shiza Kichuya kutoka upande wa kushoto.

Matokeo haya yana maanisha Benin imeshindwa kulipa kisasi cha kufungwa na Tanzania, kwani mara ya mwisho, zilipokutana Oktoba 12, mwaka 2014 Taifa Stars ilishinda  mabao 4-1, mabao ya Nahodha wa wakati huo, beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ dakika ya 16, kiungo Amri Kiemba dakika ya 39, Thomas Ulimwengu dakika ya 49 na Juma Luizio, wakati la Benin lilifungwa na Suanon Fadel dakika ya 90.

Post a Comment

0 Comments